Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 27.04.2019:Van Dijk, Tielemans, Cech, Alderweireld, Pogba, Perez, Herrera, Eriksen, Neymar

Manchester United wamemkosa Virgil van Dijk

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United walichelewa kuzungumza na Virgil van Dijk kwa ajili ya kusaini nae mkataba wa kumtoa Southampton mwezi Januari mwaka 2018, na matokeo yake wameambiwa mlinzi huyo raia wa Uholanzi anajiunga na Liverpool. (Mail)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anajiandaa kuvunja rekodi ya Foxe t kwa dau la £40m ili kumuingiza klabuni kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans mwenye umri wa miaka 21ambaye ana mkataba wa kudumu kutoka Monaco. (Mirror)

Juventus wanamfuatilia kwa karibu mlizi wa timu ya Tottenham Mbelgiji Toby Alderweireld

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juventus wanamfuatilia kwa karibu mlizi wa timu ya Tottenham Mbelgiji Toby Alderweireld

Chelsea wanajiandaa kumpatia nafasi kwneye klabu hiyo mlinda lango wa Czechoslovakia Petr Cech, mwenye umri wa miaka 36, mara tu baada ya kustaafu mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)

Juventus wanamfuatilia kwa karibu mlizi wa timu ya Tottenham Mbelgiji Toby Alderweireld, mweney umri wa miaka 30, ambaye ana weza kutoka kwenye kikosi hicho iwapo atalipa £25m. (Calciomercato)

Paul Pogba amekataa kukamilisha taratibu za visa ya klabu ya Manchester United, huku Real Madrid wakisema watamchukua

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Paul Pogba amekataa kukamilisha taratibu za visa ya klabu ya Manchester United, huku Real Madrid wakisema watamchukua

Paul Pogba amekataa kukamilisha taratibu za visa ya klabu ya Manchester United kabla ya timu hiyo kwenda kwa matembezi barani Asia, huku Real Madrid wakisema wanaimani kuwa watasaini mkataba na Mfaransa huyo anayecheza katika safu ya kati mwenyeumri wa miaka 26 mwishoni mwa msimu huu . (Sun)

Paris Saint-Germain imefikia makubaliano na mchezaji wa safiu ya kati wa Manchester United Muhispania Ander Herrera

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Paris Saint-Germain imefikia makubaliano na mchezaji wa safiu ya kati wa Manchester United Muhispania Ander Herrera

Meneja Rafael Benitez anataka Newcastle ihakikishe inabaki na Muhispania Ayoze Perez, mwenye umri wa miaka 25 ambaye kiwango chake kinathamanishwa kuwa ni £30m. Mshambuliaji huyo amedokeza kuwa yuko tayari kusikia maombi kutoka klabu nyingine zitakazotaka kumuajiri. (Mirror)

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen

Paris Saint-Germain imefikia makubaliano na mchezaji wa safiu ya kati wa Manchester United Muhispania Ander Herrera, mwenye umri wa miaka 29, ambaye atajiunga nao msimu huu. (Mail)

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen ambaye thamani yake ni £60m akiwa na umri w amiaka 27. Meneja Manager Ole Gunnar Solskjaer anamuona Eriksen kama kiungo muhimu katika mipango yake ya kuijenga upya klabu hiyo katika Old Trafford. (standard)

Mbrazili Neymar, anataka kushirikiana na Eden Hazard Chelsea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbrazili Neymar, anataka kushirikiana na Eden Ha

Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Paris St-Germain Mbrazili Neymar, mwenye umri wa miaka 27, anataka kushirikiana na Eden Hazard Chelsea , na anaamini kuwa yeye na Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 28 wanaweza ''kusababisha maafa pamoja''. (Fox Sports Brazil - via Fox Sports Asia)

Arsenal, Liverpool na Manchester United wako makini kusaini mkataba na mchezaji Adrien Rabiot ambaye kwa sasa yuko Paris St-Germain baada ya Real Madrid kujiondoa katika harakati za kumchukua Mfaransa huyo anayecheza katika safu ya katikati akiwa sasa na umri wa miaka 24 . (Mirror)

Arsenal, Liverpool na Manchester United wako makini kusaini mkataba na mchezaji Adrien Rabiot

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal, Liverpool na Manchester United wako makini kusaini mkataba na mchezaji Adrien Rabiot

Roy Hodgson amekiri kuwa Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuondoka Crystal Palacemsimu ujao. Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast amethamanishwa na Palace kwa kiwango cha £80m. (Mirror)

Mlinzi wa Manchester United kutoka Ivory Coast Eric Bailly, mwenye umri wa miaka 25, anatumai ataendelea kubaki katika klabu ya Manchester United msimu ujao, licha ya Lyon na Arsenal kuonyesha nia ya kumtaka. (MEN)

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumpatia Danny Welbeck, mwenye umri wa miaka 28, mkataba mpya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumpatia Danny Welbeck, mwenye umri wa miaka 28, mkataba mpya

Real Madrid imeipatia Chelsea fursa ya kurefusha zaidi mkataba wa mkopo na Mcroatia Mateo Kovacic mwenye umri wa miaka 24 kwa msimu ujao, licha ya kwamba the Blues watatakiwa kumnunua mchezaji mwingine kwa £26m. (Star)

Atletico Madrid wamemchoka mzaha wa Diego Costa na wanajiandaa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Atletico Madrid wamemchoka mzaha wa Diego Costa na wanajiandaa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumpatia Danny Welbeck, mwenye umri wa miaka 28, mkataba mpya. Mshambuliaji huyo wa England ambaye amekuwa nje ya uwanja tangu Novemba kutokana na majeraha , amebakiza wiki kadhaa amalize mkataba wake wa sasa na walkati huo huo West Ham, Newcastle na Everton wote wanamfuatilia kwa karibu kuona kama wanaweza kumchukua . (Mirror)

Atletico Madrid wamemchoka mzaha wa Diego Costa na wanajiandaa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa mnunuzi atakayewtoa pesa nzuri zaidi msimu huu . (Mundo Deportivo - in Spanish)

West Ham na Watford a ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazo chunguza kwa karibu mienendo ya winga wa Colombia Juan Cuadrado mwenye umri wa miaka anayechezea klabu ya Juventus. (Tuttosport - in )