Mwanamke amzalia mwanawe mtoto kwa kubeba mimba kwa niaba yake

Mwanamke ambeba mtoto mchanga

Chanzo cha picha, Ariel Panowicz / http://arielfried.com/

Maelezo ya picha, Mtoto Uma Louise na wazazi wake, Matthew Eledge na Elliot Dougherty akiwa na bibi yake, Cecil Eledge

Mwanamke wa miaka 61, mkaazi wa jimbo la Nebraska nchiniMarekani ameelezea furaha yake kwa kufanikiwa kujifungua mjukuu wake mwenyewe baada ya kubeba mimba kwa niaba ya mwanawe wa kiume ambaye yuko katika uhusiano wapenzi wa jinsia moja.

Cecile Eledge aliyebeba ujauzito wa mjukuu wake kwa niaba ya mwanawe Matthew Eledge na mume wake Elliot Dougherty alijifungua mtoto wa kike anayeitwa Uma Louise wiki iliyopita.

Bi Eledge anasema alitoa pendekezo hilo baada ya mwanawe na mume wake Dougherty kugusia nia yao ya kuanzisha familia.

"Kwanza wote walinicheka sana kwa kutoa wazo hilo," Bi Eledge aliiambia BBC.

Wakati huo Bi. Eledge, anasema alikuwa na miaka 59, na pendekezo lake lilichukuliwa kama utani na baadhi ya watu wa familia yake.

Wanandoa Eledge na Dougherty siku mtoto wao alipozaliwa

Chanzo cha picha, Ariel Panowicz / http://arielfried.com/

Maelezo ya picha, Wanandoa Eledge na Dougherty siku mtoto wao alipozaliwa

Lakini wakati wanandoa hao, Matthew Eledge na Elliot Dougherty ambao wanaishi Omaha walipokubaliana na Bi Eledge na mume wake, walianza kutafakari kuhusu mbinu tofauti za kupata mtoto kama waliyopendekezewa na mtaalamu wa masuala ya uzazi.

Bi Cecile Eledge, alihojiwa na ufanyiwa msururu wa uchunguzi wa kimatibabu, na kila kitu kiliashiria kuwa anaweza kubeba ujauzito.

Kwa kuwa mwanawe Mathew Eledge alikuwa na uwezo wa kupeana manii, dada yake Dougherty alisaidia kupatikana kwa yai la mwanamke.

Bw. Dougherty, ambaye anafanya kazi ya saluni, alisema kupata mtoto kupitia mfumo wa kisayansi unaofahamika kama IVF "ndio matumaini pekee" ya kupata mtoto wao.

"Tulitaka kuwa tofauti ndio maana tukaamua kutumia mbinu hiyo," alisema Bw. Eledge, ambaye ni mwalimu wa shule ya umma.

Cecile Eledge na mjukuu wake, Uma.

Chanzo cha picha, Ariel Panowicz / http://arielfried.com/

Maelezo ya picha, Cecile Eledge na mjukuu wake, Uma

Bw. Dougherty, ambaye anafanya kazi ya saluni, alisema kupata mtoto kupitia mfumo wa kisayansi unaofahamika kama IVF "ndio matumaini pekee" ya kupata mtoto wao.

"Tulitaka kuwa tofauti ndio maana tukaamua kutumia mbinu hiyo," alisema Bw. Eledge, ambaye ni mwalimu wa shule ya umma.

Mama Cecile Eledge anasema ujauzito wake uhaukuletea matatizo yoyote tofauti na dalili anayopata mwanamke mjamzito.

Bi Eledge pia alisema kuwa katika kipindi cha ujauzito ulikuwa ''mzuri'' akilinganisha na mimba mbili za kwanza alizobeba.

"Kila aliyepata taswira ya hatua yake alimuunga mkono na kusaidia kimawazo," alisema.

Familia ya Eledge ikiwa pamoja

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Lea Yribe, dada yake Dougherty aliyetoa yai lililokuzwa kwa njia ya kisayansi, Bw. Dougherty, Mama Cecile Eledge na mwanawe wa kiume Matthew Eledge

Bi Eledge anasema wanandoa Mathew Eledge na Dougherty walikuwa na furaha sana. ''walikuwa hawasemi jambo lingine lolote isipokuwa ni lina nitajifungua mtoto wao,"

Lakini ujauzito huo ulifichua visa vikali vya unyanyapaa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja katika jimbo la Nebraska nchini Marekani.

Japo ndoa ya wapenzi wa jinsia moja imehalalishwa katika jimbo hilo tangu mwaka 2015, Nebraska haina sheria inayolinda uhusiano wa aina hiyo.

Wanandoa Elliot Dougherty na Matthew Eledge wakutana na mtoto wao Uma hospitalini

Chanzo cha picha, Ariel Panowicz / http://arielfried.com/

Maelezo ya picha, Wanandoa Elliot Dougherty na Matthew Eledge wakutana na mtoto wao Uma hospitalini

Mathew Eledge aligonga vichwa vya habari miaka minne iliyopita alipofutwa kazi katika shule ya upili ya Skutt Catholic baada ya kuwaarifu wasimamizi wake kuhusu mpango wa kufunga ndoa na mpezi wake wa jinsia moja Bw. Dougherty.

Taarifa hiyo ilizua mjadala mkali katika jamii yake katika hatua ambayo iliwafanya wanafuzi wa sasa na wa zamazi wa shule hiyo kuzindua kampeini katika mitandao wa kijamii kupinga unyanyapaa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja "Komesha unyanyapaa dhidi ya Bw. Eledge na watu wengine kama yeye".

Kampeini hiyo ambayo sasa imefungwa iliungwa mkono na watu 102,995.

Mtoto Uma na wazazi Elliot Dougherty na Matthew Eledge

Chanzo cha picha, Ariel Panowicz / http://arielfried.com/

Maelezo ya picha, Mtoto Uma na wazazi Elliot Dougherty na Matthew Eledge

Familia, ya Bi Eledge inasema kuwa iliamua kuelezea kisa chao kama sehemu ya kukabiliana na ''chuki'' dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na familia zao kuonesha "kuna matumaini ya wao kuishi maisha ya kawaida" kama familia zingine.

"Binafsi nimeamua kutotilia maanani wanachokisema watu kuhusu ndoa yetu,"alisema Bw. Eledge.

"Mwisho wa siku tuna familia, tuna marafiki na jamii kubwa inayotujali."

Familia za Eledge na Dougherty siku alipokuzaliwa mtoto Uma

Chanzo cha picha, Ariel Panowicz / http://arielfried.com/

Maelezo ya picha, Familia za Eledge na Dougherty siku alipokuzaliwa mtoto Uma

Wiki moja baada ya mtoto Uma kuzaliwa ,Bi Eledge anasema yeye na mjukuu wake wako salama.

"Huyu mtoto atakuwa katika mazingira ya upendo," alisema bi Eledge.

"Hivi ndivyo ilivyojaaliwa kuwa."