Mambo matano yanayodhihirisha dunia 'si ya wanawake'

wanawake

Chanzo cha picha, Gallo Images

Maelezo ya picha, Mavazi kama viatu, kofia za jeshi bado ni za ukubwa wa wanaume
Muda wa kusoma: Dakika 4

Wakati safari ya wanawake watupu kwenda anga za juu ilipokatizwa katika dakika za mwisho kutokana na kubadilishwa mavazi, mjadala mkali umezuka kuhusu namna wanawake wanavyojizatiti kuwepo katika dunia inayoonekana imebuniwa wanaume.

Caroline Criado Perez, muandishi wa makala inayoangazia data inayodhihirisha upendeleo na dunia iliyobuniwa wanaume anasema hakushangazwa kuhusu mjadala huo wa mavazi ya wanawake kwenda anga za juu.

"Ndicho kinachofanyika kila uchao linapokuwa suala la tunachokibuni."

"Tumezoea kuwafikiria wanaume kila mara tunapokuwa katika ubunifu na wanawake hufikiriwa tu katika misingi ya - aina tofuati ya watu."

Haya ni mambo matano yanayodhihirisha namna dunia haikubuniwa wanawake.

Christina Koch (centre) assists fellow astronauts Nick Hague (left) and Anne McClain in their spacesuits

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Christina Koch (katikati) awasaidia wana anga wenzake Nick Hague na Anne McClain kuvaa nguo za anga za juu

1. Mavazi ya anga za juu

Shirika la anga za juu Nasa lilikabiliwa na shutuma kali katika mtandao wa Twitter lilipotangaza kwamba huedna safari ya wanawake watupu kwenda anga za juu huenda ikasitishwa kutokana na ukubwa wa mavazi hayo.

Limefafanua kwamba mwana anga za juu Anne McClain aligundua dakika za mwisho kwamba ukubwa wa mavazi aliyopewa awali ni bora kuliko aliyotarajiwa kusafiri nayo ambayo yalikuwa makubw amno, na kwa hivyo safari hiyo ilisitishwa kwa sababu za kiusalama.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space
Female soldier in field 1994

Chanzo cha picha, David Turnley via Getty Images

2. Zana za kijeshi

Mnamo 2016, jeshi la Marekani lilianza kuwasajili wanawake kupigana vita katika vitengo vilivyokuwa vya wanaume pekee katika jeshi la nchi kavu, jeshi la maji na la anga - lakini zana nyingi ziliundwa za wanaume.

Jeshi liliongeza saizi nane ndogo za ziada za wanawake mwaka huo, lakini mavazi kama viatu, kofia za jeshi bado hazijageuzwa ukubwa.

Baadhi ya wanawake wameiambia Buzzfeed News mwaka huu kwamba wakati wa wakihudumu katika jeshi, walilazimika kukarabati na kuvaa mavazi ya kinga dhidi ya mashambulio yaliobuniwa wanaume katika kuhakikisha mavazi hhayo yanawasaidia kuwakingakama inavyotakiwa.

Wanawake walilazimika kutumia nguo zilizostahili katika jeshi. Katika vita vya pili duniani inaarifiwa wanawake hawakutarajiwa kufanya kazi zisizo za ofisini.

Ndio sababu jeshi halikutayarisha sare za kazi nyingine kama fundi wa magari.

A crash test dummy at the Denver Auto Show

Chanzo cha picha, Andy Cross via Getty Images

3. Sanamu la ajali za magari

Kwa miaka mingi Marekani haikufanya majaribio ya kutosha ya ajali ya gari kwa sanamu la mwanamke aliyefungwa mshipi mpaka ilipofika mnamo 2012.

sanamu hilo la majaribio lilitumika kwa mfano wa mwanamume.

Kwa mujibu wa utafiti wa mnamo 2011 wa chuo kikuu cha Virginia Center for Applied Biomechanics, ulidhihirisha kwamba madereva wanawake waliohusika katika ajali za magari walikuwa na uwezekano wa 47% kupata majeraha mabaya wakilinganishwa na wanaume.

Na sio Marekani pekee, hali hiyo imedhihirika pia katika mataifa ya Umoja wa Ulaya.

"Katika majaribio matanao kisheria yanayofanyika katika Umoja wa ulaya kuna mmoja tu unaofafanua kwamba ni lazima utumie sanamu la kike na pia nalo huwekwa kwenye kiti cha abiria tu, " anasema Bi Criado Perez.

Anaeleza kwamba sekta hiyo inafahamu wazi kwamba ni lazima ishughulikie suala la wanawake - lakini "hawajlifanya hilo kwa namna yoyote ya maana inayodhihirisha kwamba wanawake ni 50% ya idadi jumla ya watu waliopo".

Apple iPhone XR is displayed during an Apple special event at the Steve Jobs Theatre on September 12, 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

4. Simu za kisasa

Kuanzia programu tumishi mpaka ukubwa wa simu, kuna ubunifu tofuati katika simu za kisasa uliowafanya wanawake kusema kwamba wanaume ndio waliolengwa katika ubunifu wa simu hizo.

Mikono ya wanawake kwa wastani ni mdogo kwa angalau inchi moja kuliko ile ya wanaume - jambo linalozusha tatizo kila kunapoundwa simu zenye uso mkubwa.

kutuma ujumbe katika simu yenye uso wenye ukubwa wa inchi 4.7 au kubwa zaidi huenda ikawa tatizo au kufanya kuwa vigumu kwa wanawake wengi na (baadhi ya wanaume walio na mikono midogo).

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

Taarifa zaidi:

Presentational white space
Woman works at desk

Chanzo cha picha, The Washington Post via Getty Images

5. Nafasi za kukaa ofisini

Makosa katika ubunifu au usanifu wa majengo yanayotumika kama ofisi yanadhihrika hadi katika mazingira yanayoonekena kubuniwa kupendelea maslahi ya wanaume.

Pengine hujalitilia akili hili lakini wataalamu wanasema kwa mfano ujoto wa ofisi nchini Marekani uliidhinishwa katika miaka ya 60, na ulitokana na vipimo vya mwanaume mwenye umri wa miaka 40 aliye na uzito wa kilo 70.

Utafiti wa mnamo 2015 uliochapishwa katika jarida la Nature uligundua kwamba hali ni tofauti kwa mwanamke anavyohisi ujoto ambayo ni kiwango cha chini kwa hadi 35% ikilinganishwa na mwanamume na iliyotumika katika hesabu hiyo za miaka ya nyuma na inayotoa tifuati ya nyuzi joto takriban 5.

Mwanahistoria Shirley Wajda anasema jitihada za kuwa na usawazishaji umechangia kubuniwa "dunia ambapo kimoja kinaundwa na kutarajiwa kutosha kila mtu".