Jeff Bezos: Mkuu wa Amazon akubali kulipa $35bn katika talaka

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanamume tajiri duniani, mmiliki wa mtandao wa Amazon Jeff Bezos, na mkewe MacKenzie wamefikia makubaliano ya aina yake ya talaka yenye thamani ya $35bn.
Bi Bezos anapokea 4% ya umiliki wa kampuni hiyo kubwa duniani.
Amazon iliyoasisiwa na Jeff Bezos huko Seattle mnamo 1994, mwaka mmoja baada ya wawili hao kuoana, na bi Bezos alikuwa mojawapo ya waajiriwa wa kwanza.
Wote walituma ujumbe kumhusu mwenzake baada ya tangazo hilo la kufikiwa makubaliano ya talaka.
Wawili hao hawakutoa taarifa ya ziada ya makubaliano ya kifedha yaliofikiwa.
Hisa za Amazon pekee zitamfanya Bi Bezos kuwa mwanamke wa tatu tajiri huku Jeff akisalia kuwa tajiri mkubwa duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jeff Bezos, mwenye umri wa miaka 55, na MacKenzie, wa miaka 48, walioana mnamo 1993 na wana watoto wanne.
Ujumbe wa Bi Bezo katika Twitter ni wa kwanza na wa kipekee tangu kujiunga na mtandao wa blogu mwezi huu. Katika ujunbe huo ameandika, "nimeshukuru kukamilisha talaka yangu na Jeff kwa ushirikiano wa pamoja".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Bezos kwa upande wake ameandika: "Ninawashukuru rafiki zangu na familia yangu kwa kunipa moyo na kuonyesha upendo... zaidi MacKenzie."
Aliukamilisha ujumbe huo kwa kuandika: "Ni msaidizi, anayejituma, na mwenye mapenzi, na wakati maisha yetu yanafunguka katika siku za usoni, nafahamu kwamba nitaendelea kujifunza kutoka kwake."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kabla ya makubaliano hayo Bezos alimiliki 16.3% ya kampuni ya Amazon. Ataendelea kushikilia 75% ya umiliki huo lakini Bi Bezos amewasilisha haki zake zote za maamuzi kwa mtalaka wake.
Anakabidhi pia hisa zake alizokuwa anamiliki katika gazeti la Washington Post na kampuni ya safari za anga za juu ya Bwana Bezos, Blue Origin.
Amazon ni kampuni ya mtandao inayotumika pakubwa duniani katika biashara ya mauzo.
Mwaka jana ilipata faida ya $232.8bn na imemsaidia Bwana Bezos na familia yake kukusanya utajiri wa $131bn, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
















