Maelfu ya wasichana duniani wanakabiliana na tatizo la usonji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasichana na wanawake wengi wenye usonji huwa watu wakimya sana, wenye aibu na wenye kujitenga,'' anasema Alis Rowe, Mwandishi na mjasiriamali.
Mara nyingi, anaeleza, ''hawa wasichana wakimya matatizo yao hayawezi kubainika kwa watu wengine.
Alis aliambiwa ana tatizo la usonji akiwa amekua kijana, lakini ni mmoja kati ya wanawake wachache kubainika na changamoto hiyo.
Usonji ni hali inayoathiri namna watu wanavyowasiliana na kuchangamana na watu wengine.Hali ya ufahamu wa mtu mmoja mmoja huwa ni kwa namna mbalimbali.
Inakadiriwa kuwa mtoto mmoja kati ya 160 ana usonji,kwa mujibu wa Shirika la afya duniani, lakini kuna tofauti kubwa katika kubaini tatizo hili kwa kuzingatia jinsia.
Utafiti mpya uliofanyika uingereza ambao umelenga sifa za wanawake wenye usonji unaona kuwa uwiano ni karibu 3:1
Kama hii ni kweli basi maelfu ya wasichana wanaishi na usonji bila wenyewe kujua.
Kutokufahamu tatizo

Chanzo cha picha, Getty Images
''Sikubainika kuwa na usonji mpaka nilipotimia miaka 22,'' anasema Alis.
''Nilitumia siku zote za maisha yangu nikijiuliza kwa nini niko tofauti' nikaingiwa na uoga kwa kuwa nilikua tofauti , na kujaribu kujilinganisha na wengine ili nisiwe wa tofauti.''
Lakini alipobainika kuwa na usonji maisha ya Alis yalibadilika:''kwa sasa nina sababu kwa nini niko tofauti.Inaogopesha kuwa tofauti na kutokufahamu kwa nini-ukifikiria kuwa uko peke yako.''
''Hali ya kujikubali iliyosababishwa na kukubaliana na matokeo ya uchunguzi inamaanisha kuwa nimekuwa tayari kubadili mtindo wa maisha yangu.''
''Nina uwezo wa kuwaeleza marafiki na wenzangu kuwa nina changamoto hivyo namna yangu ya kufikiri na tabia vinaweza 'visiwe vya kawaida'.''
''Mambo yote haya yameboresha afya ya akili na nimekuwa na urafiki wenye maana zaidi, na wenye kuufurahia.''
Kama ilivyo kwa Alis,watu wengi wanaona kubainika kuwa kuna tatizo la usonji kunasaidia sana kujua sababu ya mtu kujisikia anavyojisikia, kukubaliana na hali na familia na marafiki kukuelewa.
Kubainika kuwa na usonji ni muhimu sana kwa kuwa wengi walio na changamoto hii hupatwa na matatizo mengine ya akili, hofu, sonona na hata kujiumiza wenyewe.
Kwanini wasichana na wanawake wengi hawabainiki kuwa na usonji?

Chanzo cha picha, Getty Images
Dalili za usonji kwa wasichana na wanawake si sawa na zinazowapata wavulana na wanaume.Ugumu ambao watafiti wanauona kwa wasichana wenye usonji ni kuwa wasichana huwa na tabia ambazo zinaonekana kukubalika au kuzoeleka kama vile kuwategemea wengine,kutoshiriki kwenye baadhi ya vitu au hata kuwa na huzuni.
Wanaweza kupenda vitu ambavyo kwao ni vitu rahisi kuvifanya, kwa mfano hawatapendezwa sana na masuala ya teknolojia na hesabu.
Msichana kwa kawaida hawi mtukutu au mwenye kutoa chagamoto,hivyo hakuna anayeweza kuwabaini,'' anasema Alice.
Ugumu katika kufanyiwa uchunguzi

Chanzo cha picha, Getty Images
Daktari alipomuona Alis aliorodhesha akieleza kwa nini anafikiria kuwa ana usonji na kutaka afanyiwe uchunguzi.
Lakini inakuwaje kama ugekuwa mtoto? inakuwaje kama huwezi kujieleza mwenyewe?
''Walipogundua kuwa mwanangu ana usonji nilipata ahueni kubwa,'' anaeleza Marilu.
''Lakini kivipi mzazi atajisikia ahueni wakati mtoto wake wa miaka 10 anagundulika na tatizo la usonji?
Marilu alihangaika miaka kadhaa akitafuta daktari na walimu waweze kujua tatizo la binti yake, Sophia.
Ikiwa wazazi na wanaowaangalia watoto watakua na taarifa kuhusu namna ya kuishi na usonji kungeweza kuboresha maisha ya watu wenye usonji.

Chanzo cha picha, Getty Images
''Binti yangu Sophia ana aibu , lakini ni mbunifu sana, hivi ndivyo namna mwalimu wake anavyomuelezea,'' anasema Marilu.
''Nilijua mapema kuwa ilikua vigumu kwake kuwa na marafiki wa umri wake.Alikua mdogo wa mwili ukilinganisha na wenzake.
''Nilihisi alikua hivyo kwa kuwa wenzake wanamuona yuko tofauti, mpaka pale nilipogundua kuwa anapata shida shuleni, wakati wa kulala huniambia ''sina marafiki mama'' hakuna anayenipenda'.''
''Nilikua nikimuambia kuna siku nzuri na siku mbaya, lakini nilikua nawauliza waalimu wake kama wamegundua kitu chochote shuleni,'' alisema Marilu.
'' Jibu mara zote lilikua hilo hilo: 'Hakuna kinachoendelea'.''
Lakini hali iliendelea kua mbaya kisha Marilu alirudi kwa waalimu.
''Nilichukia sana.Niliwauliza kama Sophia alikua akionewa shuleni.Nilijua kuna tatizo.Lakini niliambiwa kuwa ni mawazo yangu tu na hisia zangu kali', Nikashutumiwa kuwa ninamdekeza.''
Marilu na familia yake walikuwa wakipambana kujua nini kinachoendelea, wote walikua wanahangaika : ''Mara nilimwambia rafiki yangu kuwa kumpeleka Sophia shuleni ni kama nampeleka kuchinjwa
''Katika kipindi cha mwezi mmoja nilimuona mwanangu akiwa mwenye hasira na kama aliyevurugikiwa.akijifanya kuwa sawa nje lakini akirudi ni mtu mwenye kupoa sana.''
''Nilijua Sophia ana tatizo na sikuweza kumsaidia.Nilijaribu nikashindwa.Bahati mbaya, hisia zangu zikawa msaada wangu.Labda ningeweza kueleza kilichomsibu mwanangu nikiwa na ushahidi,kuliko hisia, tungeweza kugundua tatizo mapema,'' anasema Marilu.












