Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uingereza: Baadhi ya wasichana huchomwa moto matiti yao yachelewe kukua
- Author, Na Amber Haque
- Nafasi, BBC Victoria Derbyshire
Elimu kuhusu athari za 'kuunguza matiti' yapaswa kuwa ya lazima kwenye mtaalaa wa shule kuzuia mabinti kufanya au kufanyiwa vitendo hivyo, Taasisi ya Elimu nchini Uingereza imeeleza.
Vitendo hivyo vinahusisha kuunguza matiti ya wasichana kwa kutumia vitu vya moto ili kuzuia matiti yasikue haraka, ili kutowavutia wanaume.
Mbunge wa chama cha Conservative Nicky Morgan amesema waalimu lazima wapewe elimu , kwa kuwa wana nafasi kubwa katika kutoa elimu hiyo kwa wasichana
Wizara ya mambo ya ndani imesema waalimu wanawajibu wa kutimiza lengo hilo.
'Ni mwiko kulia'
"Kinaya" - Ambalo si jina halisi anaishi nchini Uingereza.
Familia yake yenye asili ya Afrika Magharibi-ambako vitendo vya kuunguza matiti vilianzia-alianza kufanyiwa vitendo hivyo akiwa na umri wa miaka 10.
Alisema mama yake alimwambia ''kama hautayaunguza, wanaume wataanza kukufuata ili ufanye nao ngono''
Iko wazi mama wa mtoto ambaye atakua akimuuguza bintiye matiti, hutumia mawe au kijiko. Huviunguza kwenye moto kisha huvikandamiza, na kusugua kwenye matiti.
Vitendo hivi vinaweza kufanyika kwa miezi kadhaa.
''Maumivu yake huwa ya muda mrefu,'' Kinaya alieleza.
''Huruhusiwi hata kulia, ikiwa utafanya hivyo wanasema utailetea aibu familia, itatoa ishara kuwa wewe si mchana jasiri''.
Kinaya kwa sasa amekua mtu mzima na mwenye watoto wakike.
Mtoto wake mkubwa alipotimiza miaka 10, mama yake Kinaya alipendekeza mjukuu wake huyo aunguzwe matiti.
''Nilisema hapana, hapana,hapana, hakuna mtoto wangu yeyote atapitia nilichokipitia, na kuniathiri mpaka sasa kutokana na niliyoyapitia.
Tangu wakati alipoondoka na kwenda mbali na familia yake, akiamini kuwa kuna madhara makubwa ikiwa atawaunguza matiti bila ridhaa yao.
Inaaminika kuwa takriban wasichana 1,000 nchini Uingereza wameathirika na uchomaji matiti.
Lakini wakati kuna elimu kuhusu ukeketaji dhidi ya wasichana, kuna hofu watu wachache wanafahamu kuhusu uchomaji moto matiti.
Mwanamke mmoja amekiambia kipindi cha Victoria Derbyshire kuwa aligundua kua kuunga matiti si kitu cha kawaida alipojigundua kuwa ana muonekano tofauti na wenzake shuleni, hali iliyomuathiri kisaikolojia.
Nicky Morgan amesema masuala ya uchomji matiti yanapaswa ''kukabiliwa, kuelezwa na kukomeshwa kabisa''.
Wale walio karibu na wasichana ni budi wakufundishwa kutambua kuwa kuchoma matiti hufanyika Uingereza, na kuweza pia kuwashauri wasichana hatua wanazopaswa kuchukua
Mwanake mmoja ''Simone'', alikiambia kipindi cha Victoria Derbyshire kuwa alichomwa matiti akiwa na miaka 13 mama yake alipogundua kuwa ana mahusiano ya jinsia moja.
''Kwa mujibu wa mama, nilikua navutia kwa sababu ya matiti yangu, hivyo ikiwa atanichoma , nitachukiza na hakuna atakayekua akinitamani.''
Alichomwa matiti kwa kipindi cha miezi kadhaa.
Alitakiwa kuvaa kitambaa cha kubana sana kuzunguka kifua hali iliyosababisha kupata ugumu wakati wa kupumua.
Miaka michache baadae, alipopata mtoto na mwanaume ambaye alilazimishwa kuolewa naye, kukawa na shida iliyodumu kwa muda mrefu
''Nilipata taabu sana wakati wa kunyonyesha''
''Nilihisi kama baadhi ya neva kuwa zimeharibiwa.''
'uhalifu unaofichwa'
Hakuna sheria yeyote ya kupinga vitendo hivi, lakini wizara ya mambo ya ndani inaeleza vitendo hivyo ni unyanyasaji dhidi ya watoto.
Angie Marriot, daktari wa zamani wa maradhi ya wanawake anasema tatizo hili lilikua haliripotiwi.
Amesema ni uhalifu unaofanyika kwa kificho sana.
kwa mara ya kwanza wamezungumza kilichowatokea na kueleza kuwa waliogopa kujitokeza kwa kuona aibu.
Simone bado anaugulia makovu aliyoyapata, na anataka kutoa elimu kuhusu uhalifu huu.
''Ni udhalilishaji, inaumiza na kukuondolea utu wako,'' Alieleza.
''huwezi kujihisi mwanadamu.''