Je upi mustakabali wa uhusiano baina ya Ugiriki na Uturuki?

uturuki politics
Maelezo ya picha, Rais Edogan

Viongozi na washirika wawili wa nchi za Magharibi Ugiriki na Uturuki, wamefanya mazungumzo huko Ankara kwa jitihada za kuboresha uhusiano baina yao.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja , baadaye, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alirejelea wito wake wa kutaka ushirikiano zaidi kutoka nchini Ugiriki katika juhudi za kujaribu kuwakabidhi watuhumiwa nafasi ya kushiriki katika jaribio la mapinduzi nchini Uturuki mnamo Julai 26 mwaka jana.

Erdogan alinukuliwa akisema, 'Tunalileta tena kwa makini kwa marafiki zetu wa Kigiriki tukiwa na matumaini tena, tukitarajia zaidi ushirikiano kutoka kwa majirani zetu Ugiriki'.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni askari wanane wenye asili ya Uturuki ambao waliomba ukimbizi nchini Ugiriki wakati jaribio la mapinduzi liliposhindwa.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, yuko katika ziara yake ya pili katika kipindi cha miaka minne, alisisitiza uungaji wake mkono kwa Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Pande zote mbili zilizungumzia haja ya makubaliano ya kawaida katika kisiwa kilichogawanyika cha Kupro, ambacho kiligawanyika kati ya Wagiriki wengi na waturuki wachache tangu mwaka 1974.