Jeshi la Israel limekishambulia kikosi cha Quds cha jeshi la Iran nchini Syria

Syrian air defences said intercepting reported Israeli missiles in Damascus, 21 January

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Vikosi vya ulinzi wa angani Syria vinasema vimezuia makombora ya Israel
Muda wa kusoma: Dakika 2

Jeshi la Israel linasema limeanza kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Iran nchini Syria.

Kikosi cha ulinzi Israel (IDF) kinasema operesheni yake ni dhidi ya kikosi cha Quds - kikosi maalum katika jeshi la mapinduzi la Iran.

Haikutoa ufafanuzi zaidi. Lakini kuna taarifa kuhusu makombora yaliofyetuliwa katika maeneo yanayo uzunguka mji mkuu wa Syria, Damascus mapema Jumatatu.

Vyombo vya habari nchini Syria vinasema vikosi vya ulinzi wa angani vimezuia 'shambulio la Israel'. Siku ya Jumapili jeshi la Isarel lilisema limezuia kombora katika eneo la Golan Heights.

Tunafahamu nini kuhusu operesheni hiyo?

Kikosi cha Israel IDF kilitangaza kuanza kwa operesheni hiyo kupitia ujumbe wa tweeter mapema leo Jumatatu.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Televisheni ya taifa nchini Syria Sana imenukuu duru katika jeshi kwamba kikosi cha ulinzi wa angani nchini humo kimedhibiti 'makombora kutoka kwa adui'.

Shirika linaloangalia haki za binaadamu nchini Syria lililo na makao yake nchini Uingereza (SOHR) linasema makombora ya Israeli yalikuwa yanalenga "maeneo ya mji mkuu Damascus".

Watu walioshuhudia mjini Damascus wanasema walisikia milipuko mikubwa angani usiku.

Shirika hilo la SOHR baadaye lilieleza kwamba makombora ya Israel yameharibu maghala ya silaha na kambi za kijeshi zinazomilikiwana Iran na kundi linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah.

SOHR limeongeza kwamba kuna watu waliofariki kutokana na shambulio hilo.

Map showing Israel, Lebanon and Syria

Onyo la Netanyahu

Operesheni hiyo inajiri baada ya Israeli kusema kwamba 'kombora la roketi lililofyetuliwa kaskazini mwa eneo la Golan Heights na lilidhibitiwa na mfumo wa ulinzi ".

Eneo ambalo ni kivutio kikubwa msimu wa baridi katika mlima Hermon katika eneo hilo la Golan Heights lilifungwa kutokana na yaliotukia.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alitoa onyo kali wakati wa ziara yake nchini Chad hapo jana Jumapili.

"Tuna sera iliyopangwa, kulenga maeneo yanayodhibitiwa na Iran nchini, na kumdhuru yoyote aliyejaribu kutudhuru," alisema.

Ni nadra kwa Israel kukiri kueteleza mashambulio katika maeneo nchini Syria.

Lakini mnamo Mei 2018, Israel ilisema ilishambulia karibu miundo mbinu yote ya kijeshi ya Iran huko katika shambulio lake kubwa tangu kuanza kwa vita vya kiraia nchini Syria mnamo 2011.