Mahakama ya DR Congo yaidhinisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu aitisha maandamano

Felix Tshisekedi akiwapungia mkono wafuasi wake baada ya kutangzwa mshindi wa uchgauzi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Felix Tshisekedi Naongoza chama kikubwa cha upinzani nchini leads DR Congo kilichoanzishwa na babake

Mahakama ya katiba DR Congo imemuidhinisha rasmi Felix Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo.

Mgombea aliyechukua nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa urais nchini DR Congo Martin Fayulu ameitaka jamii ya kimataifa kutotambua matokeo hayo na ameitisha maandamano.

Taarifa yake inajiri baada ya ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha ushindi wa mgombea mwengine wa upinzani , Felix Tshisekedi .

Muungano wa Afrika ulisema siku ya Ijumaa kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa.

Bwana fayulu sio mgombea pekee ambaye anaamini kwamba yeye ni muathiriwa wa wizi wa kura huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi.

Haijulikani iwapo raia wataheshimu wito wa Fayulu wa kufanya maandamano.

Siku ya Jumatatu ujumbe wa AU unatarajiwa Kinshasa na unatarajiwa kukutana na mtu anayedaiwa 'kuiba' kura rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila.

Iwapo Tshisekedi ataapishwa , muungano wa AU utaamua iwapo utamtambua au la.

Mahakama ya kikatiba nchini DR Congo imeidhinisha ushindi wa mgombea wa urais katika uchaguzi huo Felix Tshisekedi.

Mahakama ilikataa ombi la rufaa iliowasilishwa na Martin Fayulu ambaye ni mgombea mwengine katika uchaguzi huo wa mwezi Disemba 30.

Martin Fayulu.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Martin Fayulu anasisitiza kuwa yeye ndiye aliyechaguliwa rai

Bwana Fayulu alihoji kwamba Bwana Tshisekedi alikuwa amefanya makubaliano ya kugawana mamlaka na rais Joseph Kabila, hatahivyo upande wa Tshisekedi umekana hilo.

Licha ya uamuzi wa mahakama hiyo, bwana Fayulu alisema kuwa yeye ndio mshindi wa uchaguzi huo wa urais.

Bwana Fayulu pia alihoji kwamba jamii ya kimataifa haitambui matokeo rasmi ya uchaguzi huo.

Muungano wa Afrika AU ulisema siku ya Ijumaa kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo ya uchaguzi huo.

Mahakama ilisemaje?

Mahakama ilisema kuwa bwana Fayulu alishindwa kuthibitisha kuwa tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo bandia.

Iliendelea na kumtanagaza Felix Tshisekedi kuwa rais aliyechaguliwa kwa wingi wa kura. Sasa anatarajiwa kuapishwa katika kipindi cha siku 10 zijazo.

Ghasia zimetokea kila kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi katika taifa hilo.

Lakini thibtisho la matokeo rasmi ya uchaguzi huenda likaonyesha kubadilika kwa uongozi kihalali tangu DR Congo ijipatie uhuru wake kutoka kwa taifa la Ubelgiji 1960.

Uhamisho wa utawala
Presentational white space

Je uchaguzi wa Disemba 30 ulikuwaje?

Tume ya uchaguzi awali ilikuwa imetangaza kwamba felix Tshisekedi alikuwa amepata asilimia 38.5 ya kura hiyo huku Fayulu akijpatia asilimia 34.7.

Mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary alipata asilimia 23.8.

Hatahivyo Fayulu alihoji kwamba bwana Tshisekedi alifanya makubaliano na Bwana Kabila ambaye amekuwa uongozini kwa miaka 18.

Bwana Kabila alikuwa haruhusiwi kuwania muhula mwengine kikatiba.

Uchguzi huo ulikuwa ufanyike mwaka 2016 lakini ukaahirishwa kutokana na matatizo ya mipango, maafisa walisema.

Kulikuwa na visa vya kuchelewa kwa shughuli ya kupiga kura siku ya kupiga kura.

Kutofanya kazi kwa baadhi ya vifaa vya kielekroniki vya kupiga kura katika baadhi ya vituo vya kupiga kura ni mojawapo ya changamoto.

Je wengine wanasemaje?

Matokeo rasmi yamepingwa na kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa ambalo linasema kuwa lilisambaza wachunguzi 40,000 wa uchaguzi kote nchini.

Wataalam wa kimataifa kutoka nchini Marekani pamoja na mataifa ya Ufaransa na Ujerumani poa yameonya wasiwasi wao.

Wakati huohuo Umoja wa mataifa unasema kuwa vita vya kikabila magharibi mwa nchi hiyo vimesababisha vifo vya watu 890 katika kipindi cha siku tatu mwezi ulioipita.

Ghasia baina ya jamii za Banunu na Batende zilianza katika vijiji vinne katika eneo la Yumbi kati ya tarehe 16 na 18 Disemba kulingana na Umoja wa mataifa.

Idadi kubwa ya watu katika maeneo hayo wamewachwa bila makao ikiwemo takriban watu 16,000 waliopata hifadhi kwa kuvuka mto Congo na kuingia katika taifa jirani la Congo BrazzaVille.