Mwanamke raia wa Indonesia araruliwa na mamba mkubwa hadi kufa Sulawesi

Mwanamke mmoja raia wa Indonesia ameuawa na Mamba huko Sulawesi baada ya kuanguka karibu nae.

Deasy Tuwo, 44, inasemekana alikuwa akimlisha Mamba huyo kwenye shamba huko Sulawesi mahali anapofanyia kazi na sehemu ambayo mamba huyo alihifadhiwa bila kibali.

Mamba huyo mwenye kilo 700 aitwae Merry inasemekana alimng'ata mkono na sehemu kubwa ya tumbo.

Mnyama huyo amehamishiwa katika hifadhi wakati mamlaka ikimtafuta mmiliki.

Bi Tuwo alikuwa ni msimamizi wa maabara katika eneo hilo na alikuwa akimpatia chakula Merry tarehe 10 mwezi januari ambapo aliangukia mikononi mwamnyama huyo.

Wafanyakazi wenzie waliuona mwili wake asubuhi ya siku inayo fuata.

Hendriks Rundengan kutoka katika hifadhi ya maliasili kaskazini mwa Sulawesi ameiambia BBC indonesia kuwa maafisa walejaribu kutembelea shamba hilo mara kadhaa ili kuwaondoa mamba hao lakini hawakuwahi kuruhusiwa kuingia ndani.

"Tumekuja hapa mara kadhaa lakini sikuzote tunakuta pamefungwa," alisema katika mahojiano siku ya jumatano.

Kwa mujibu wa AFP, mamlaka inaamini kwamba sehemu ya viungo vya mwanamke huyo vitakuwepo ndani ya Mamba huyo mwenye urefu wa mita 4.4

Kwa sasa polisi wanajaribu kumsaka mwanaume mwenye uraia wa Japani ambaye anamiliki shamba na Mamba huyo.

Hifadhi ya archpelago Indonesia nu nyumbani kwa Mamba wa aina mbali mbali ambao mara kwa mara wamekuwa waki vamia na kuuwa binadamu, AFP inaripoti.

Mwezi april 2016, mtalii kutoka Urusi aliuliwa na mamba katika kisiwa cha Raja Ampat, sehemu maarufu ya michezo ya majini mashariki mwa archpelago, inaripoti.

Duniani Mamba wanakadiriwa kuuwa takribani binadamu 1000 kwa mwaka, wengi zaidi ya papa.

Mamba kawaida hawaweki mitego ya kuwinda binadamu bali wao ni wauaji wa kutumia fursa.

Afrika pekee kuna mamia ya kesi za kuvamiwa na mamba kwa mwaka.