Wapinga sanamu la shetani lenye 'upole' Uhispania

Chanzo cha picha, City of Segovia
Sanamu la shetani linalopangwa kuwekwa katika mji wa Uhispania Segovia limeshutumiwa kwa kufurahi sana.
Sanamu hilo la shaba bronze liliundwa kwa heshima ya ngano au hadithi ya kale inayosema kuwa shetani alihadaiwa kujenga bomba mashuhuri la maji mjini humo.
Lakini wakaazi wanasema shetani huyo - anayetabasamu na anayeonekana kupiga slefie na simu ya mkononi - anaonekana kuwa na upole na urafiki mwingi.
Msanii huyo ameiambia BBC ameshangazwa na kiwango cha shutuma zilizoelekezwa kwa kazi yake.
Jaji mmoja sasa ameagiza sanamu hilo lisiwekwe kwa sasa wakatianaposhauriana kufahamu iwapo linadhalilisha Wakristo.
Zaidi ya watu 5,400 - takriban asilimia 10% ya idadi ya watu wa mji huo - wamtia saini rasimu wakitaka sanamu hilo lisiwekwe.
Barua hiyo inasema kwasbabau sanamu hilo la shetani linaoenakana likitabasamu sana huku likishika simu mkononi, ni kana kwamba 'linatukuza uovu', na hivyo basi 'linadhalilihsa wakatoliki'.

Chanzo cha picha, City of Segovia

Mzozo huo umemshangaza sana msanii aliyeunda sanamu hilo, José Antonio Abella.
"Imenishangaza kwamba watu wanapinga sanamu hili la shetani kutoa heshima kwa hadithi maarufu ambayo watoto wa Segovian wamehadithiwa na kufunzwa shuleani," Abella, ameiambia BBC.
"Naipenda Segovia. Nimeishi hapa kwa miongo mitatu na nilitarajia kuwa sanamu hili lingedhihirisha shukrani zangu kwa Segovia, kwa kuwa mji nilokokulia."
Diwani wa mji huo Claudia de Santos ametaja muitikio huo kuwa"sio wa haki na wa kuvunja moyo".
Amesema atajaribu kuhakikisha kwamba sanamu hilo litawekwa kama ilivyopangwa.













