Chatu aliyegandamwa na kupe 500 atibiwa kwa upungufu wa damu

A close-up of Nike the carpet python

Chanzo cha picha, CURRUMBIN WILDLIFE HOSPITAL

Maelezo ya picha, Chatu aliyepewa jina la utani Nike, amebanduliwa kupe waliomganda

Nyoka aliyetolewa kupe wapatao 500 waliokuwa wamemgandama mwilini mwake, amedhoofika na anaugua upungufu wa damu, madkatrai Australia wanasema.

Nyoka huyo aliokolewa kutoka kwenye kidimbwi cha kuogelea huko Gold Coast, Queensland wiki iliyopita.

Nyoka huyo aliyepewa jina Nike, alitibiwa na madaktari wa wanyama kwa 'maambukizi makali'.

"[Hili] huenda limemsababisha kutoweza kutambaa, na kusababisha kupe hao kumganda," Hospitali ya Currumbin Wildlife Hospital imesema katika taarifa yake.

Carpet python covered in ticks in a Queensland pool

Chanzo cha picha, Gold coast and brisbane snake catcher/facebook

Maelezo ya picha, Madaktari wa wanyama wanasema wamewatoa kupe 511 kutoka mwilini mwa nyoka huyo

Shirika la wanyapa pori linasema linatumai kumuachia nyoka huyo katika miezi ijayo.

Kwa sasa yuko na muuguzi aliye na ujuzi, hospitali imesema.

"Nike hajapata nafuu kikamilifu, lakini tunatumai atapona kikamilifu".

Kupe huweza kusababisha upungufu wa damu mwilini kutokana na kuinyonya damu ya mnyama mwilini.

Koala aliyegandamwa na Kupe

Hospitali imesema hivi maajuzi pia ilitibu mnyama aina ya Koala aliyepatakana akiwa amegandamwa na kupe zaidi ya 100.

A tick-affected joey koala receiving a blood transfusion

Chanzo cha picha, CURRUMBIN WILDLIFE HOSPITAL

Maelezo ya picha, Iliwachukua madaktrai saa mbili kuwabandua kupe kutoka kwenye Koala huyu

Koala huyo alitengana na mamake alipookolewa, na huenda alikuwa na jeraha lililomlazimu kukaa chini na kugandamwa na kupe hao, wamesema wanaharakati wa kimazingira.

Wataalamu wanasema ni kawaida kwa wanyama kugandamwa na kiasi kidogo cha kupe na wadudu wengine.

Hatahivyo, iwapo mnyama ni mgonjwa wa kudhoofika, wadudu hao wanaweza kuzaana na kuongezeka kwa haraka na kuuzidi nguvu mfumo wa kinga mwilini mwa mnyama huyo.