Roger the kangaroo: Sababu ya Australia kumuomboleza kangaroo mwenye miaka 12

Roger, a kangaroo

Chanzo cha picha, Kangaroo Sanctuary Alice Springs

Muda wa kusoma: Dakika 2
Presentational white space

Roger, kangaroo aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na unene wake na misuli yake iliyotuna vilivyo ambayo angekuwa binadamu tungelisema alikuwa na 'six-pack', amefariki dunia akiwa na miaka 12.

Wapenzi wa wanyama nchini humo wamekuwa wakiomboleza kifo chake.

Kangaroo huyo aliokolewa angali mdogo kutoka porini baada ya mamake kuuawa katika ajali ya barabarani.

Alikulia katika kituo cha kuwatuza kangaroo cha Kangaroo Sanctuary eneo la Alice Springs nchini Australia.

Roger, a kangaroo

Chanzo cha picha, Kangaroo Sanctuary Alice Springs

Alinenepa haraka sana - na kufikia wakati wa kifo chake alikuwa na kimo cha 2m (6ft 5) na uzani wake ukawa 89kg. Akiwa amesimama, alikuwa mrefu kuliko binadamu wengi.

Roger, a kangaroo

Chanzo cha picha, Kangaroo Sanctuary Alice Springs

Kituo hicho cha kuwatunza kangaroo kilisema mnyama huyo alifariki wikendi kutokana na 'uzee'.

Walisema walikuwa wamempoteza "mvulana mtanashati".

Ruka Facebook ujumbe

Haipatikani tena

Tazama zaidi katika FacebookBBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje.

Mwisho wa Facebook ujumbe

Presentational white space

Chris "Brolga" Barns, anayesema alianzisha kituo hicho cha kuwahifadhi kangaroo kutokana na Roger na "wake zake kadha" anasema mnyama huyo alikuwa ndume mtawala katika kituo hicho kwa miaka mingi.

"Alikuwa na kuwa kangaroo aliyependwa na watu kutoka kila pembe ya dunia, sawa na tulivyompenda sisi," alisema.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Presentational white space

Bw Barns anasema Roger amezikwa katika hifadhi hiyo ili "daima aendelee kuwepo hapa."

Umaarufu wa Roger duniani ulianza mwaka 2015 baada ya picha zake akiiponda ponda ndoo ya maji iliyotengenezwa kwa chuma kwa mikono yake, huku misuli yake iliyotuna vilivyo ikionekana wazi.

Katika uzee wake, alihangaishwa na ugonjwa wa yabisi kavu ambao huathiri mifupa na maungio na pia alianza kupofuka.

Lakini alikuwa anafurahia "maisha yake ya uzeeni", alisema Bw Barns mwaka 2016.

Porini, kangaroo kwa kawaida huishi hadi miaka 10 hivi lakini wakiwa kwenye hifadhi wanaweza wakaishi miaka zaidi ya hiyo.