Picha za wanyama za kuchekesha zaidi 2017

Chanzo cha picha, Penny Palmer/ Barcroft Images
Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya dubu wanaoonekana kukoleza uhusiano wao pamoja na nyingine ya sili.
Picha hizi ziliteuliwa kushindania tuzo za picha za ucheshi za wanyama mwaka huu, katika vitengo vitano.
Jumla ya picha 3,500 ziliwasilishwa kwa mashindano hayo.
Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.

Chanzo cha picha, Tibor Kercz/ Barcroft images
Mshindi wa jumla Tibor Kercz kwa picha hii yake ya bundi anayeonekana kuhitaji usaidizi kujishikilia vyema kwenye tawi mti alitunukiwa kikombe ambacho kilitengenezwa na wanaume na wanawake wenye ulemavu kutoka Tanzania.
Kadhalika, alipewa vifaa zaidi vya kupigia picha.
Alishinda pia tuzo kwenye kitengo cha picha ya kuvutia zaidi ya mtandaoni pamoja na kujishindia safari ya kwenda mbugani Kenya.
Kabla ya picha hii ya Andrea Zampatti kushinda kitengo cha picha za ardhini, picha hii yake ya panya anayeonekana kuangua kicheko ilisambazwa sana mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.

Chanzo cha picha, Andrea Zampatti /Barcroft Images
Na ingawa bahari ni kubwa, picha hii iliyoshinda kitengo cha picha za chini ya bahari inaonesha viumbe wanaweza bado kukaribiana sana.

Chanzo cha picha, Troy Mayne/ Barcroft Images
Kitengo cha picha za angani, picha hii ya njiwa mmoja wao akionekana kufuata njia ya moshi wa ndege, iliyopigwa na John Threlfal Preston, Lancashire ndiyo iliyoshinda.

Chanzo cha picha, John Threlfal/ Barcroft Media
Hapa chini ni baadhi ya picha nyingine zilizofanya vyema.

Chanzo cha picha, Carl Henry/ Barcroft Images

Chanzo cha picha, Olivier Colle/ Barcroft Images

Chanzo cha picha, Daisy Gilardini/ Barcroft Media

Chanzo cha picha, Jean-Jacques Alcalay/ Barcroft Images

Chanzo cha picha, Bence Mate/ Barcroft Images

Chanzo cha picha, George Cathcart/ Barcroft Images













