Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jay Z na Lady Gaga ni miongoni mwa wanamuziki waliosusia kushiriki katika filamu ya R. Kelly
Jay z na Lady Gaga ni mongoni mwa wanamuziki maarufu ambao walikataa kuonekana katika filamu inayoonyesha maisha halisi ya R.Kelly , mtayarishaji wa filamu hiyo ameeleza.
Makala hiyo ya 'Surviving R Kelly', ilizinduliwa jana nchini Marekani ikiwa imeangazia madai ya unyanyasaji wa kingono ambayo yamekuepo dhidi yake kwa miongo kadhaa ambapo amekataa kuusika na madai yote.
John Legend ni mwanamuziki pekee aliyekubali kuhojiwa .
Mwezi Desemba 2018, mfululizo wa Makala hiyo uliondolewa baada ya watu kuanza kupata simu za vitisho.
Muandaaji wa Makala hiyo , Dream Hampton alisema kuwa ilimuwia vigumu kupata watu mashuhuri kushirikiana na R.Kelly ili iweze kuendelea.
"Tulimuomba Lady Gaga , Erykah Badu ,Celine Dion, Jay-Z, Dave Chappelle na wote walikuwa muhimu kwake," lakini Hampton hakuhamini kwa nini hawakumuunga mkono yeye wala jitihada zake.
John Legend ndio mwanamuziki pekee ambaye alikubali kushiriki katika mfululizo wa Makala hiyo ambapo ataonekana katika mfululizo wa mwisho wa filamu hiyo utakaoneshwa kesho.
"R Kelly amesababisha maumivu mengi kwa watu," Hampton alisema.
Muimbaji ambaye alikuwa anasifika kwa uimbaji , Hampton alimuita 'shujaa' licha ya kuwa jina hilo alilikataa.
Kwa kila mtu kuniambia nilipata ujasiri gani kuonekana katika makala hiyo lakini mimi sikuona hatari yeyote",John alisema.
Pamoja na kuwa mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa katika historia ya muziki wa R&B, Kelly amekuwa akisakamwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa ngono tangu mwaka 1990.
Makala hilo imefafanua uhusiano aliokuwa nao na mwanamuziki Aaliyah mwaka 1994, ambapo alimuoa Aliyah akiwa na umri wa miaka 15 wakati yeye akiwa na umri wa miaka 27.
Na badae jarida la Vibe lilibaini kuwa Aaliyah alikuwa amedanganya umri wake katika cheti cha ndoa kwa kuandika kuwa ana umri wa miaka 18.Ndoa hiyo ilifutwa mwezi Februari mwaka 1995.
Hivi karibuni mama yakeAliyah, Diane Houghton alitoa maoni yake alipohojiwa katika makala moja na kudai kuwa shutuma zote ni za uongo.
"Mume wangu alikuwa anasafiri na Aaliyah na alikuepo kwenye mahojiano yote na sehemu zote ambazo Aliyah alizuru kwa ajili ya muziki,"
Mfululizo wa filamu hiyo umeonyesha mke wa zamani wa R Kelly aiyejulikana kama Andrea, ambaye pia alitoa madai ya unyanyasaji.
Mwaka 2018, R Kelly alizindua wimbo wenye dakika 19 unaoitwa 'Admit' ambao ulijibu madai kadhaa dhidi yake dhidi ya ngono.