Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Harusi ya kifahari ya mabilionea inayosubiriwa India, Beyoncé afanya tamasha
Mwanamuziki Mmarekani Beyoncé amefanya tamasha kwenye sherehe za kifahari zinazokaribisha harusi kubwa nchini India.
Isha Ambani, binti ya wa mwanamume tajiri zaidi nchini India anafunga ndoa na Anand Piramal, mtoto wa bilionea mwingine wiki hii.
Beyoncé alikuwa mmoja wa watu wengi mashuhuri pamoja na mastaa wa Bollywood na watu kama Hillary Clinton.
Harusi hii inakuja wakati harusi zingine kadha za hivi majuzi zinazoshindania umaarufu na ubora.
Familia ya Ambani yenyewe hivi majuzi ilihudhuria harusi ya wacheza filamu wa Bollywood Deepika Padukone na Ranveer Singh.
Wikendi iliyopita Isha Ambani alikuwa mmoja wa wasimamizi kwenye harusi ya mwanafilamuaPriyanka Chopra na muimbaji Mmarekani Nick Jonas.
Siku kamili ya harusi ya binti wa bilionea Mukesh Ambani ni Jumatano lakini sherehe zimeanza za kuelekea kwa harusi hiyo zilianza wikendi.
Huenda ikawa moja ya ndoa ya ufahari wa juu zaidi nchini India na wageni wengi ni pamoja na mama wa zamani wa taifa nchini Marekani na mgombea urais wa mwaka 2016 Hillary Clinton, mmiliki wa vyombo vya habari Arianna Huffington, mchezaji kriketi Sachin Tendulkar bilionea Lakshmi Mittal.
Kulinganna vyombo vya habari wageni wamesafirishwa kwa safari kwa ndege 100 zilizokodishwa.
Beyoncé aliiangaia jukwaani siku ya Jumapili usiku kwa sherehe kwa jina sangeet, wakati wa muziki na densi kabla ya harusi.
Alisambaza picha zake kwenye akaunti yake ya Instagram.
Malipo yake hayakutangazwa kwa umma lakini hilo halitakuwa tatizo kwa familia ya Ambani. Mukesh Ambani mkurugezi mkuu wa Reliance Industries ana utajiri wa dola bilioni 47.
Mara ya mwisho ndoa ya famiali ya mfanyabiashara raia wa India ilipata umaarufu kama huu ilikuwa mwaka 2004.
Harusi zingine za kifahari za raia wa India
Mzaliwa wa India na bilionea anayeishi mjini London Lakshmi Mittal aliandaa harusi ya binti yake nchini Ufaransa. Gharama yote ya harusi hiyo zikiwemo zawadi kwa familia na marafiki ilifikia hadi dola milioni 55 wakati huo.
Lakini mastaa wengine wa Bollywood na marafiki kwa familia ya Ambani na mara nyingi huonekana wakihudhuria karamu zilizoandaliwa na familia hiyo.
Deepika Padukone na Ranveer Singh
Familia ya Ambani yenyewe ilihudhuria harusi ya hivi majuzi ya wanafilamu wa Bollywood Deepika Padukone na Ranveer Singh; na Isha Ambani alikuwa msimamizi kwenye harusi ya Priyanka Chopra iliyofanyika Jodhpur jimbo la Rajasthan.
Eneo ambapo harusi ya Ambani na Pirimal itafanyiwa huko Udaipur ni mji wa karne ya 16. Ni nyumbani mwa hoteli zenye ufahari wa juu zaidi nchini India.
Ni mji mdogo wenye uwanja wa ndege mtulivu lakini utakuwa wa shughuli nyingi wakati huu.
Padukone na Singh
Harusi wa Padukone na Singh ilifaninyiwa eneo moja la kifaharai kwenye ziwa moja nchini Italia ambapo Bi Ambani na Bw Pirimal walifanyia posa ya lakini ilifuatiwa na sherehe zingine nne nchini India
Mavazi ya Padukone yalijumuisha kuanzia yale ya kitamaduni hadi yale yaliyoshonwa na mwamitindo wa mavazi kutoka Lebanon Zuhair Morad.
Mavazi ya wawili hao yalifanana - kama hayakufanana kwa rangi basi yangekuwa tofauti kabisa.
Sonam Kapoor na Anand Ahuja
Harusi ya nyota wa Bollywood Sonam Kapoor na mfanyabiashra Anand Ahuja mwezi Mei ilisambazwa kwa njia ya kipeke kwennye mtandao wa Instagram. Sonam ambaye alitajwa kuwa anayependa mitindo mara kadhaa alibadilisha mavazi kwa jioni moja na hatua hiyo yake ikapataumaarufu mkubwa.
Wale waliohudhuriaa karamua walichapisha video za wanachezafilamu na watu mashuhuri wakicheza densi huku mmoja akiimba vibaya video amboyo ilisambaa sana mitandaoni.