Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama kilichogunduliwa kwenye kaburi la kale nchini Misri
Mambo ya kale ya kaburi linalokisiwa kuwa la zaidi ya miaka 3,500 yamegunduliwa Misri.
Wana akiolojia walioshirikiana na chuo cha Ufaransa cha Strasbourg walifanya ugunduzi huo katika bonde la Assasseef karibu na mjini wa Laxor.
Majeneza mawili ya miili yaligunduliwa.
Pia wana akiolojia hao waligundua karibu vifaa 1,000 vya kale.
Kaburi hilo linaaminiwa kutoka miaka ya 1550 BC na 1300 BC.