Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Man City 3-1 Man Utd: Wenyeji washikilia ushindi na kusalia kileleni katika Derby
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema ushindi wa Manchester City katika mchuano wa derby ulitokana na usaidizi wa mechi za "kirafiki" katika wiki iliyopita.
City ilirudi katika kilele cha ligi kuu England au Premier League wakati magoli ya David Silva, Sergio Aguero na Ilkay Gundogan yakiipatia klabu hiyo buingwa pointi tatu katika uwanja wa Etihad.
Lakini Mourinho anasema wenyeji hao walikuwa na faida kutokana na kwamba mechi zake mbili - ya nyumbani dhidi ya Southampton na Shakhtar Donetsk ambapo timu hiyo ilishinda kwa jumla ya 12-1 - ilikuwa ni ushindi wa wazi ikilinganishwa na mechi ilizocheza timu yake hivi karibuni.
Hii ni mechi ya tatu kucheza nje kufutia ushindi mtawalia walipokaribishwa na Bournemouth na Juventus wiki iliyopita
Ushindi wa City haukuwana shaka baada ya Silva kutinga goli la mapema kuipa timu hiyo faida ya mapema.
Walitinga la pili na la uzito kupitia tobwe alilosukumua Aguero na kumpita David de Gea dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya kubadilishana pasi na Riyad Mahrez.
Kikosi cha Mourinho ambacho hakikumjumuisha Paul Pogba aliyekuwa nje kwa jeraha hakikuonekana kuwa tishio kubwa.
Matumaini yamalizika kwa Man United kunyanyua taji
Mourinho ametetea timu yake kuanza mchezo kwa kasi ndogo msimu huu na anaonekana ameshindwa kupata tiba ya hilo.
Waliponea chupuchupu mara kadhaa kabla ya Silva kufunga bao la kwanza kunako dakika 12 hatua iliyoipatia City udhibiti.
Ni wazi kikosi kilimkosa Pogba aliyejeruhiwa, aliyesaidia kuibadili taswira katika mechi ya Derby msimu uliopita, lakini kwa mara hii ubunifu na mashambulio hayakudhihirika kwa man United.
Na wakati goli la Gundogan likisifiwa, Mourinho alitazama kwa hasira wakati walinzi wa United waliposimama kama milingoti tu.
United sasa wapo nyuma kwa pointi 12 nyuma ya City. Inavyoonekana walisahahu taji la Premier kwa muda uliosaliwa katika msimu huu.
Nyota wa mechi David Silva (Manchester City)
'Tulicheza tukiwa na makosa ' - walichosema
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola akizungumza na Match of the Day: "Tulitaka tucheze vizuri mbele ya mashabiki wetu na tunajua umuhimu wa kucheza mechi hii. Tulicheza vizuri [katika nusu ya pili ] na goli la Sergio Aguero lilitusaidia sana kufikia kumalizika awamu ya kwanza."
Bosi wa Manchester United Mourinho akizungumza na Sky Sports: "Tulikuwa tumejizatiti hadi kunako dakika ya 80na kitu na goli la tatu lilivunja matumaini ya kikosi.
"Mmoja anadhani ni mchezo mbaya mwingine anafikiria ni mechi iliyokuwa na makosa.
"Tupo nje ya timu nne za juu, tunaweza kulizungumzia vipi taji? Tung'ang'ane kuliziba pengo kuingia katika nafasi ya nne bora, kisha tutazame tofuati."