Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 11.11.2018: Pogba, Mourinho, Guardiola, Sterling, Ramsey, Suarez, Sancho
Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 25 ameimarisha uhusiano wake na meneja wa klabu Jose Mourinho. (Manchester Evening News, via Raisport)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola aliingilia kati mkataba wa Raheem Sterling kuhakikisha kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 anasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Sunday Mirror)
Chelsea wanataka kumsaini mchezaji mwenye miaka 24 kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez ambaye meneja wa Blues Maurizio Sarri alijaribu kumsaini wakati wake kama meneja wa Napoli. (Daily Star on Sunday, via Marca)
Arsenal wana mpango wa kumbadilisha kiungo wa kati Aaron Ramsey, 27, na mshambuliaji wa Roma Patrik Schick, 22, mwezi Januari. (Daily Star on Sunday, via Corriere dello Sport)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe ana hofu kuwa beki mwenye miaka 23 Nathan Ake ambaye amehusishwa na Manchester City, Manchester United na Tottenham atauzwa na anatafuta mchezaji wa kuchukua nafasi yake. (Sun on Sunday)
Beki wa Liverpool Andy Robertson atararajiwa kuongeza mshahara wake hadi pauni 60,000 kwa wiki wakati anakaribia kusiani mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo. (Sunday Mirror)
Mkataba wa mlinzi wa Manchester United Phil Jones unamalizika msimu ujao lakini klabu lazima ifanye uamuzi kuuongeza kwa mwaka mmoja huku Arsenal and Tottenham wakimmezea mate mchezaji huyo wa maaka 26. (Sun on Sunday)
Barcelona walikataa hata kuzungumzia uwezekani wa Everton kumsajili kiungo wa kati Andre Gomes, 25, kwa mkataba wa kudumu wakati Tottenham walimsaini kwa mkopo msimu wote wakati wa msimu wa joto. (Liverpool Echo)
Wing'a wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18 anasema hawezi kutupa muda kwa mabadiliko ikiwa ataulizwa kuhusu kuhama. (Sunday Express, via Bild)
Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, anasema hana furaha kuhusu kulengwa na wapinzani wakati anaanzz kuhisi madhara ya kucheza mpira. (Sunday Telegraph)
Tamaduni huko Arsenal imebadilika tangu meneja Unai Emery achukue mahala pake Arsene Wenger, kwa mujibu wa kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan, 29. (Sunday Telegraph)
Bora kutoka Jumamosi
Inaripotiwa kuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ya Uingereza raia wa Chile, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 29, anataka kuachana na klabu hiyo ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu ajiunge nayo akitokea klabu ya Arsenal. ( Times).
Beki wa kulia wa klabu ya Manchester United, Muitaliano Matteo Darmian ana uwezekano mkubwa wa kuondoka kwenye klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi January, ambapo klabu za Inter Milan na AS Roma zimeonesha nia ya kumtaka. (Sun).
Mlinda mlango wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Ubelgiji Simon Mignolet mwenye umri wa miaka 30 anawindwa na kocha wa klabu ya Nice ya Ufaransam Patrick Viera. (Het Belang van Limburg, via Mirror).
Klabu ya Huddersfield inajiandaa kutoa ofa kwa mlinda mlango wa klabu ya Burnley, Tom Heaton mwenye umri wa miaka 32, ambaye amepoteza nafasi kwenye timu yake baada ya raia mwenzake wa Uingereza Joe Hart kupewa nafasi. (Sun).
Klabu za Manchester City na FC Barcelona huenda zikakosa kumsajili beki wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Ajax mwenye umri wa miaka 19, Matthijs de Ligt ambaye anahusishwa sana na kukubali ofa ya klabu ya Juventus ya Italia. (Calciomercato).
Klabu ya Chelsea ya Uingereza itashindana na timu kadhaa za Italia ikiwemo Juventus kutaka kupata saini ya kiungo wa klabu ya Brescia, Sandro Tonal ambaye thamani yake inatajwa kufikia Euro milioni 20. Kiungo huyu mwenye umri wa miaka 18 tayari amefananishwa na kiungo wa zamani wa Italia Andrea Pirlo. (Goal).
Wamiliki wa klabu ya Aston Villa ya Uingereza watafikiria uwezekano wa kuubadili uwanja wa wao ifikapo mwaka 2019 wakati huu wakiendelea na mipango ya baadae ya klabu hiyo, mipango ambayo huenda ikahusisha pia uuzaji wa haki za jina la uwanja ambao umekuwa uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 1897. (Birmingham Mail).