Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yapendekeza sheria ya kupiga marufuku wahamiaji haramu
Wahamiaji wanaoingia nchini Marekani kupitia mpaka wa kusini hawatapewa hifadhi tena chini ya sheria mpya ya uhamiaji, utawala wa Trump umesema.
Tangazo hilo lilitolewa na idara ya haki na usalama wa kitaifa linasema sheria hiyo mpya itakomesha visa vya wahamiaji waliyokiuka sheria kuingia Marekani.
Rais ana uwezo wa kupiga marufuku wahamiaji kwa ''maslahi ya taifa'' ilisema tangazo hilo.
Suala la uhamiaji lilikuwa ajenda kuu ya kampeini ya rais Trump katika uchaguzi wa mwaka 2018 wa katikati ya muhula.
Trump amekuwa akikabiliana na msafara wa maelfu ya wahamiaji kutoka Amerika ya Kati ambao wamekuwa wakitaka kuingia nchini Marekani kupitia mpaka wa kaskazini.
Aliamuru majeshi kushika doria katika mpaka huo kama hatua aliyosema ni ya kulinda nchi dhidi ya ''wavamizi''
Kaimu mwanasheria mkuu Matthew Whitaker na mkuu wa usalama wa kitaifa Kirstjeb Nielsen walitangaza kile kinachojulikana kama sheria ya mpito siku ya Alhamisi.
Katika taarifa ya pamoja viongozi hao walisema rais ana ''mamlaka ya kufutilia mbali uhamiaji wote''endapo wahamiaji watakiuka vikwazo vinavyodhibiti shughuli zao.
Pia wanasema hilo linaweza kufanyika ikiwa uwepo wao nchini utahatarisaha usalama wa Wamarekani.
Rais Trumpa anatarajiwa kuidhinisha agizo hilo kuwa sheria.
Hatua hiyo imepingwa vikali na muungano unaotetea haki ya raia ukisema ''inakiuka sheria''.
Maafisa wa muungano huo walisema "Sheria za Marekani zinawaruhusu watu kuomba hifadhi wakiwa nchini mwao ama wakiwa katika kituo cha mpakani''
Chini ya katiba ya Marekani wahamiaji wana haki ya kusikilizwa hasa wanaposema wanahofia usalama wao katika taifa waalotokea.
Wale wanaotafuta hifadhi huwa watoroka nchini mwao kwa kuhufia maisha yao.
Chini ya sheria ya kimataifa watu hao wanatambuliwa kama wakimbizi.
Mhamiaji anayetafuta hifadhi ambaye sasa anasadikiwa kuwa nchini Marekamu kwa njia haramu- pia anashathili kusikilizwa
Juhudi zilizopita za utawala wa Trump kukabilia suala la wahamiaji zimekosolewa vikali kisiasa na kisheria
Mwezi Juni mwaka huu rais alitia saini amri ya utendaji kuahidi "kuweka familia pamoja" katika kituo cha kuwashikilia wahamiaji, baada ya wazazi na watoto kutenganishwa
Siku kadhaa baadae mahakama ya juu zaidi ilidumisha marufuku ya usafiri iliyotolewa na utawala wa Trump dhidi ya mataifa kadhaa ya Kiislamu.
Mwanzoni mahakama kadhaa ziliamua kwa hatua hiyo ilikiuka katiba ya marekani.