Bodi ya Manchester United bado inamkubali Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ataendela kuisaidia bodi ya klabu licha ya hali inayoendela sasa.

Mchuano wa United dhidi ya Newcastle utakaofanyika Old Trafford utaweza kubainisha namna ambavyo United inaweza kuwafanikisha kupita mechi tano bila ya ushindi kwa awamu ya pili tangu 1998.

Mfumo wa klabu kwa sasa umejikita vikali kwenye uvumi wa matarajio ya hapo baadae ya meneja wa zamani wa Chelsea na Real madrid

Hata hivyo, inaeleweka hakuna tishio la haraka kwenye nafasi yake.

Manchester United imeeelekeza kuwa matokeo ya leo ndio yatakayoamua kuhusu Mourinho kubaki au kuondoka kwenye hiyo klabu licha ya ripoti ya mgongano wa nyuma uliopo ndani ya timu.

Mwishoni mwa juma lililopita ,United ilifungwa 3-1 dhidi ya West Ham .Matokeo ambayo yaliiweka mashetani wekundu katika nafasi mbaya ya kuanza kampeni ya ligi kwa miaka 29.

Matokeo hayo mabaya yalijumuishwa na mgogoro wa uhusiano uliopo kati ya Mourinho na kiungo Paul Pogba kuchukua vichwa cha habari vya magazeti mengi.

Baada ya kukutana na Newcastle siku ya jumamosi, watakutana na Chelsea kwenye premier league EPL,Juventus kwenye Champions league mara mbili na pia pambano dhidi ya Manchester city kwenye orodha ya wiki sita zijazo.

Hata hivyo nahodha wa zamani wa United Gary Neville ,amekosoa vikali bodi ya klabu baada ya kutangazwa Mourinho kufukuzwa kama matokeo ya mchezo dhidi ya Newcastle yatakuwa mabaya kwa United.

Neville aliiambia Sky Sports kuwa amekasirishwa sana na wazo la kumfukuza kwa kusisitiza kuwa kuna uozo kwenye msingi wa maamuzi ya klabu.