Tsunami Indonesia: Picha zilizopigwa kwa juu zaonesha athari za tetemeko na hali ya manusura

Chanzo cha picha, Reuters
Siku tano baada ya tetemeko kubwa la ardhi na tsunami iliyopiga mji wa Palu nchini Indonesian, picha hizi zinaonyesha hali halisi ya uharibifu uliotokea.

Kwa mujibu wa mamlaka ya maafa imeeleza kuwa idadi ya watu waliokufa katika eneo hilo inakadiriwa kuwa ,1300.
Chama cha msalaba mwekundu kimekadiria kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wameathirika wakati Umoja wa mataifa unasema kuwa ni watu wapatao 200,000 wana uhitaji wa haraka wa msaada.
Tathmini ya uharibifu inayoonyeshwa na ramani ya dharura iliyotolewa na Umoja wa ulaya inakadiria majengo 3,000 kuharibika katika janga hilo.

Watu wengi walikuwa ufukweni wakijiandaa kwa ajili ya tamasha wakati upepo mkubwa ulipopiga katika muda wa nusu saa au saa moja baada ya tetemeko la ardhi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maeneo yote ya jirani kama Balaroa yametandwa na na matope.
Kuna baadhi wanakadiria kuwa nyumba 1,700 zilisombwa na upepo mkali mpaka Balaroa na nyingine mamia zilisombwa mpaka Petobo.
Miongoni mwa waliokufa 30 walikuwa wanafunzi katika kundi la kikristo la masomo ya biblia.
Mchanganyiko wa taka na mchanga uliongeza shinikizo lililotokana na tetemeko la ardhi uliosababisha mpasuko na kusomba majengo na miundombinu yake.


Eneo la mlimani liliachwa na matope na kusababisha udongo ushuke chini:

Chanzo cha picha, Reuters
Tsunami imesababisha shughuli zote katika mji wa Palu kusimama.
Kuna uhaba wa chakula na maji ya kunywa pamoja na nishati.Udhibiti wa usafi wa mazingira ni tatizo linaloongezeka.Kuharibika kwa njia kunasababisha changamoto ya usafiri ambayo inakwamisha jitihada za uokoaji.

Daraja la Jemalam lenye urefu w mita 126 na futi 410 ambalo linawakutanisha watu wapatao 350,000 wa upande wa magharibi na wale wa upande wa mashariki limeharibika.

Watu wamekuwa wamekuwa wakiviokota vitu kwenye uchafu ili kupata chochote ambacho kinaweza kuwasaidia ili kufanya maisha yao yawe rahisi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa sababu vitu kama makopo ya plastiki au vifaa vya vikoni ninaweza kuwasaidia

Chanzo cha picha, AFP
Miili mingi ya waliokufa ilizikwa katika makaburi ya pamoja.Lakini inahofiwa kuwa kuna miili mingine ipo bado chini ya uchafu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi limechukua sehemu ya uwanja wa ndege ili kusafirisha misaada na watu walioumia sana.
Maelfu ya watu walikuwa wanasubiri ndege za kibiashara ili kuondoka katika mji huo wa Palu.

Chanzo cha picha, Getty Images















