Melania Trump: Atarajiwa Kenya kutoka Ghana katika ziara yake ya kwanza Afrika

Melania Trump

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Melania Trump anaangazia mradi wa lishe bora kwa watoto
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mke wa rais Trump, Melania Trump ameanza rasmi ziara yake barani afrika kwa kutembelea hospitali moja katika mji mkuu Accra nchini Ghana.

Ziara hiyo ambayo pia itamfikisha katika mataifa ya Kenya, Malawi na Misri inakuja licha ya kauli tata iliyotolewa na rais Trump, mwezi Februari mwaka huu dhidi ya mataifa ya Afrika.

Bi Melania ataangazia masuala ya afya na elimu katika harakati ya kuimarisha baadhi ya migawanyiko inayoshuhudiwa katika jamii.

Melania Trump (kushoto) akiwa na mama Taifa wa Ghana Rebecca Akufo-Addo (kulia)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Melania Trump (kushoto) akiwa na mama Taifa wa Ghana Rebecca Akufo-Addo (kulia)

Mke wa Trump anafanya nini?

Melania ameungana na mwenyeji wake mama taifa wa Ghana Rebecca Akufo-Addo, kutembelea hospitali ya Ridge mjini Accra, ambako mpia anatarajiwa kuangazia kampeini yake Be Best inayolenga kukabiliana na masuala ya unyanyasaji mitandaoni kwa ustawi wa jamii

Ghana kwa ushirikiano na shirika la USAID imekuwa ikijishughulisha na masuala ya afya kwa kusaidia mikakati ya kuimarisha afya ya kinamama na watoto wachanga pamoja na kuwahamasisha kinamama hao umuhimu wa kuzingatia lishe bora.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo Melania Trump alisema ''Najivunia sana kutembelea mataifa manne mazuri barani Afrika''.

Mkurugezi wake wa habari Stephanie Grisham amesema ''Bi Melania amechagua mataifa hayo kwa sababu kila moja itaandikisha historia ya kivyake katika ziara hii''.

watoto wa shule wakimkaribisha Melania

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watoto wa shule Ghana

Melania amepokewaje?

Mke wa Trump alipokelewa kwa vifijo katika uwanja wa ndege lakini hakujakuwa na mkutano wa hadhara.

Mwandishi wa BBC Thomas Naadi, mjini Accra anasema ujio wake umepokelewa kama siku nyingine yoyote ya kawaida.

Kumekuwa na maoni tofauti kuhusu ziara yake Ghana. Mmoja wa wakaazi wa Accra ameiambia BBC kuwa "Nafikiria Melania ni mwanamke mzuri. Historia yake hasa ni ya kutia moyo''.

Lakini wengine walimlinganisha na Bi Michelle Obama wakisema aliwavutia zaidi alipozuru Ghana na mume wake Barak Obama mwaka 2009.

Mtazamo wa rais Trump kwa Afrika ni upi?

Licha Melania Trump kuwaambia wanahabari kwamba yee na mume wake wanapenda Afrika na kwamba bara hilo ni sehemu nzuri sana duniani kumekuwa hisia tofauti kuhusiana na hilo.

Hii inafuatia matamshi anayodaiwa Trump alitoa faraghani dhidi ya mataifa ya Afrika mwezi Februari.

Bwana Trump alishutumiwa kwa ubaguzi wa rangi racism, baada ya kuripotiwa kwa kutumia neno ''shimo la choo'' kuangazia mataifa ya Afrika akizungumzia sera ya uhamiaji.

Muungano wa Afrika ulimtaka aombe radhi kwa kutoa kauli hiyo.

Baadaye aliwaambia wanahabari kuwa "Mimi si mbaguzi mkinilinganisha na mtu mwingine yeyote mbaguzi mshawahi kumhoji."

Rais wa Marekani Donald Trump

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump

Mwezi Agosti mwaka huu rais Trumpa aliikasirisha serikali ya Afrika Kusini kwa kudai kwamba kuna mauaji makubwa ya wakulima wenye asiili ya kizungu nchini Afrika Kusini.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Serikali ya Afrika Kusiini ilikanusha madai hayo

Haijabainika ikiwa bwana Trump ashawahi kuzuru bara la Afrika kabla achaguliwe rais wa Marekani su kuwa na uhusiano wowote wa kibiashara na Afrika.

Sera ya Marekani kwa Afrika ni ipi?

Rais Trump hajaipatia umuhimu mkubwa bara la afrika tangu aingie madarakani, lakini amewahi kuwaalika marais wa Misri, Nigeria na Kenya, katika ikulu ya Marekani.

Waziri wake wa kwanza mambo ya nje Rex Tillerson, alipozuru Afrika mwezi Machi aliangazia alisema kauli mbiu ya ziara yake ilikuwa kukabiliana na ugaidi,democrasia, utawala, biashara na uwekezaji.

Bwana Tillerson alionya mataifa ya Afrika dhidi ya ushirikianao wa kiuchumi na Uchina.

Pia alitangaza msaada wa dola milioni 533 kama msaada wa kibinadamu kutoka Marekani.

Utawala wa Trump umekua mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi hasa kwa makundi yenye itikadi kali nchini Somalia na eneo la Sahel

Marekani imezindua kambi ya ndege zisizokuwa na rubani nchi Nige ambayo inasimamiwa na shirika la upelelezi la Marekani, CIA.