Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Majina ya watoto: Je jina Muhammad ndio maarufu zaidi duniani?
Oliver lilitangazwa kuwa jina maarufu zaidi miongoni mwa wavulana kwa mwaka wa nne mfululizo, lakini baadhi ya wasomaji waliuliza iwapo kuna watoto zaidi walio na jina Muhammad.
Pia walitaka kujua ni majina gani yaliopewa wavulana na wasichana kwa kiwango sawa na iwapo ni lini jina Doris lilikuwa maarufu.
Haya hapa majibu yake
Je Muhammad ndio jina maarufu miongoni mwa wavulana?
Jina Oliver lilishikilia umaarufu wa kuwa jina lenye umaarufu zaidi miongoni mwa wanaume tangu mwaka 2013, kulingana na ofisi ya takwimu za kitaifa, Idadi kubwa ya wasomaji waliuliza iwapo kuchanganya pamoja herufi za jina Muhammad kutamaanisha kwamba watoto zaidi wangepewa jina hilo badala ya Oliver.
Muhammad , ni jina lenye herufi ililopatiwa watoto waliozaliwa 2017, lilikuwa la 10 kwa umaarufu miongoni mwa wavulana kwa jumla.
Oliver aliongoza orodha ya 2017 likiwa na watoto 6,259 huku watoto walio na jina Muhammad wakisajiliwa kuwa mara 3,691 bila kuongeza majina yaliongezwa kama vile Muhammad-Ali.
Iwapo tutajumlisha herufi 14 tofauti ikiwemo data tutapata wavulana 7,307 ambayo ni zaidi ya 1000 kushinda jina la Oliver.
Tofauti ni Muhammad, Mohammed, Mohammad, Muhammed, Mohamed, Mohamad, Muhamad, Muhamed, Mohamud, Mohummad, Mohummed, Mouhamed, Mohammod and Mouhamad.
Hatahivyo herufi hizo uhisabika tofauti na inayaoorodhesha tofauti kulingana na jina la mtu linavyojitokeza katika cheti cha kuzaliwa.
Kuchanganya herufi za jina fulani kunaharibu orodha hiyo, kwa mfano kujumlisha majina ya Sophie, Sophia na Sofia katika orodha ya wasichana ya 2015 kutaondoa jina la Amelia ambalo ndilo lililokuwa likiongoza kwa umaarufu.
Takwimu zinasema kuwa kujumlisha majina yalio na herufi za kufanana kunahitaji mtu kufanya uamuzi mwafaka kuhusu iwapo baadhi ya majina yana tofauti ama la. Kwa mfano watahitajika kuamua iwapo kuchukulia majina ya Sara na Sarah kama majina tofauti licha ya kwamba watu wengi huyatamka tofauti.
Je ni jina gani lililo na umaarufu mkubwa katika jinsia zote mbili?
"Je ni jina gani linalotumiwa na jinsia zote mbili likiwa na idadi sawa ya wavulana na wasichana wanalolitumia .
Avery lilikuwa jina maarufu lililotumiwa na jinsia zote mbili likiwa na idadi sawa ya wavulana na wasichana.
Kulikuwa na majina 28 katika orodha ya wavulana 6,164 na wavulana 7,508 ambayo yalipatiwa idadi sawa ya jinsia zote mbili.
Avery lilikuwa jina maarufu lililopewa jinsia zote 2017 . Lilipatiwa watoto 130 , ikiwemo wavulana 65 na wasichana 65. Jina hilo liliorodheshwa la 851 miongoni mwa wavulana 581 na 637 miongoni wa wasichana mwaka 2017.
Ni lini ambapo jina Doris lilikuwa maarufu miongoni mwa wasichana?
Doris lilikuwa miongoni mwa majina kumi bora kati ya mwaka 1904 na1944.
Jina hilo liliorodheshwa la tatu 1904 na1914, na kuwa katika nafasi ya saba 1924 na 33rd mwaka 1934.