Viongozi wa Ethiopia na Eritrea wasaini mkataba wa kudumu wa amani

Viongozi hawa wawili walitembeleana katia nchi zao katika kile kinachotajwa kuimarisha zaidi uhusiano ambao uliporomoka kwa miongo miwili
Maelezo ya picha, Viongozi hawa wawili walitembeleana katia nchi zao katika kile kinachotajwa kuimarisha zaidi uhusiano ambao uliporomoka kwa miongo miwili

Viongozi wa Ethiopia na Eritrea wametia saini mkataba wa amani tukio lililoshuhudiwa na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz katika mji wa Jeddah.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres na maafisa wa umoja wa Afrika pia walikuwemo katika tukio hilo muhimu.

Mambo muhimu yaliyoainishwa kwenye mkataba huo bado hayajawekwa wazi.

Hii inakuja miezi miwili baada ya Rais wa Eritrea Isaias Afewerki na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kusaini mkataba mwingine wa amani wa kumaliza uhasama uliodumu kwa takriban miongo miwili na kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili jirani.