Teknolojia ya kujikinga na kipindupindu Yemen

Picha ikionesha jinsi mfumo huo mpya unavyotumika

Chanzo cha picha, MET OFFICE

Maelezo ya picha, Picha ikionesha jinsi mfumo huo mpya unavyotumika

Mfumo mpya unaobashiri ni eneo gani ambalo mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu unaweza kutokea umesababisha kupungua kwa idadi ya watu wanaougua ugonjwa huo nchini Yemen.

Mfumo huo ambao unahusisha pia utabiri wa hali ya hewa, kwa kutumia kompyuta umekuwa ukiangazia taarifa za eneo kama vile msongamano wa watu, upatikanaji wa maji safi na masuala mengine yanayoendana.

Mfumo huu mpya unaotumia kompyuta unawafanya wafanyakazi wa misaada kuangazia zaidi wiki kadhaa kabla ya kutokea mlipuko katika kuudhibiti ugonjwa.

Mwaka uliopita, kulikuwa na zaidi ya wagonjwa wapya elfu 50 kwa muda wa wiki moja na kwamba mwaka huu idadi hiyo imeshuka na kufikia kiasi cha wagonjwa 2500.

Daktari akipima wagonjwa Yemen

Chanzo cha picha, UNICEF

Maelezo ya picha, Daktari akipima wagonjwa Yemen

Wanasayansi wanaamini kuwa njia hiyo inaweza kutumiwa pia kuokoa maisha katika maeneo mengine duniani.