Mkuu wa jeshi la polisi wa zamani Uganda Kale Kayihura ashtakiwa Makindye

Chanzo cha picha, AFP
Aliyekuwa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Uganda IGP - Kale Kayihura amefikishwa katika mahakama ya jeshi ya Makindye kwa mashtaka kadhaa dhidi yake.
Ameshtakiwa kwa kushindwa kulinda zana za kivita.
Kwamba kati ya mwaka 2010 na 2018 alitoa idhini silaha zitolewe kwa watu wasiostahili, na ameshtakiwa kwa kusaidia na kuhamishwa kiharamu kwa raia wa Rwanda walio uhamishoni.
Kayihura amekana mashtaka yote matatu.
Mawakili wake wameomba aachiliwe kwa dhamana, na wakatakiwa wawasilishe ombi hilo kwa maandishi.
Alikamatwa nyumbani mwake katika kijiji cha Katebe wilayani Lyantonde district mnamo Juni na amekuwa kizuizini kwa miezi miwili kufikia sasa.
Jenerali Kale Kayihura, ambaye kwa wakati mmoja aliyekuwa mojawapo ya watu wenye nguvu nchini Uganda amekuwa akizuiliwa katika kambi ya kijeshi huko Makindye, kitongoji cha mji mkuu Kampala.
Baada ya kuwasili ndani ya gari la jeshi la polisi Kayihura aliongozwa hadi ndani ya mahakama hiyo iliyokuwa imejaa watu pomoni.
Alionekana akitabasamu kiasi huku akiwa amevalia magwanda ya jeshi la taifa Uganda People's Defence Forces UPDF Ijumaa asubuhi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Usalama wa hali ya juu uliimarishwa katika maenoe ya mahakama hiyo tofuati na siku za kawaida huku watu wate waliokuwa wakiwasili wakikagulia kwa kina mlangoni.
Nje ya mahakama hiyo kulikuwana kundi la wafuasi wa kiongozi huyo wa zamani wakiwa wamevaa fulana zenye picha na ujumbe wa kuonyesha kumuunga mkono Kayihura.
Jenerali Kayihura alikuwa mkuu wa jeshi la Polisi kwa takriban miaka 12 kabla ya kutimuliwa na amiri mkuu wa jeshi Rais Museveni.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Katika muda wake wa uongozi kama mkuu wa jeshi la polisi, idadi ya maafisa wa polisi iliongezeka zaidi ya marudufu.
Jenerali Kayihura, ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.
Lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama.
Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda yalionekana kufurahia hatua ya kutimuliwa kwa Kayihura, wakisema jeshi la polisi lilikuwa limeshindwa kulinda usalama wa raia na mali zao chini ya uongozi wa Kayihura.
Kayihura anatarajiwa kurudi tena mahakamani tarehe 4 Septemba.














