Wanafunzi 4 wa Uganda wavumbua mbinu ya aina yake ya kutambua Malaria

Maelezo ya video, Wanafunzi 4 wa Uganda wavumbua mbinu ya aina yake ya kutambua Malaria

Takriban nusu ya idadi ya watu duniani wamo katika hatari ya kuugua Malaria. Ni ugonjwa unaowaua takriban watu nusu milioni kila mwaka. Lakini wanafunzi wanne wa Uganda wamevumbua kifaa hichi cha ukaguzi kinachotajwa kuwa hatua muhimu katika vita dhidi ya Malaria katika miaka ya hivi karibuni.