Nasa imetaja wanasayansi watakaosafiri angani mwaka ujao

Astronauts

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Wanasayansi hao tisa watapata mafunzo makali kuhusu mitambo watakayotumia angani

Shirika la anga la Marekani NASA limewataja wanasayansi ambao watafanya safari za anga za juu kwa kutumia vyombo vya kampuni za binafsi kuanzia mwaka ujao.

Wanasayansi hao watasafiri angani kwa kutumia vyombo vya kampuni za Boeing na SapaceX.

Aliyekuwa kamanda kwa safari ya mwisho iliyofanywa na chombo cha Nasa, Chris Ferguson, kwa sasa ni mfanyakazi wa Boeing na amehusika pakubwa kati kufanikisha chombo kitakachotumiwa kwa safari hiyo kwa jina CST-100 Starliner capsule.

Artwork: Dragon and Starliner

Chanzo cha picha, SPACEX/BOEING

Maelezo ya picha, Chombo cha SpaceX's Dragon (kushoto) kitatangulia kile cha Boeing cha Starliner (kulia) kusafiri angani.

Kwa kipindi cha miaka saba, roketi za Urusi ndizo zimekuwa zikitumiwa kuwasafirisha watu kwenda angani.

Msimamizi wa Nasa Jim Bridenstine aliwatangaza wanasayansi hao wakati wa sherehe iliyofanyika huko Johnson Space Center, Houston, Texas.

Starliner

Chanzo cha picha, BOEING

Maelezo ya picha, Kampuni hizo pia zimetengeneza mavazi yao

Wale watakaokuwemo ni pamoja na na Ferguson mwenyewe, Eric Boe na Nicole Aunapu Mann.

Chombo cha kampuni ya SpaceX cha Dragon capsule kinatarajiwa kufanya safari yake ya kwanza April mwakani kikitumia rokeri ya Falcon 9 kutoka Kennedy Space Center.

Kitakuwa na wanasayansi Doug Hauley na Bob Behnken.