Namna ugonjwa hatari wa kaswende unavyoua watoto Australia

Chanzo cha picha, SA HEALTH AND MEDICAL RESEARCH INSTITUTE
Kwa chini ya muongo mmoja uliopita, madaktari nchini Australia walikuwa na imani kuwa wanakaribia kabisa kuutokomeza ugonjwa wa kaswendekatika jamii asilia nchini humo humo, kulingana na kituo cha kitaifa cha juhudi za kupambana na Kaswende.
Tangu wakati huo, hata hivyo maradhi hayo hatari yanayoendezwa kwa njia ya ngono yameongezeka na kuwa katika kiwango cha mlipuko katika majimbo matatu na maeneo mengine.
Madaktari wanasema kuwa watoto wachanga wamekufa kutokana na maambukizi ya kaswende tangu mwaka 2011.
katika kipindi hicho hicho wanasema, mlipuko uliowaathiri kwa kiasi kikubwa jamii ya watu asilia nchini Australia umeongezeka kutoka 120 na kufikia hadi watu zaidi ya 2,100.
Wataalamu wa afya wameutaja mlipuko huu kuwa katika kiwango cha mzozo , wakisema taifa linakabiliwa na ''kazi kubwa'' ya kudhibiti tatizo hilo
Nini kinaendelea?

Chanzo cha picha, WUCHOPPEREN HEALTH SERVICE
Wengi wanaougua kaswende ni vijana wa jamii ya watu asilia kutoka Aboriginal na Torres Strait Islande wanaoishi katika mikoa ya kaskazini na kati mwa nchi , kulingana na madaktari.
Wataalam wa afya ya jamii za watu asilia, akiwemo Prof James Ward walitoa wito katika jarida kitabibu la Australia mwaka 2011 kujaroibu kumaliza kaswendekatika jamii ambamo lilikuwa ni tatizo .

Chanzo cha picha, SA HEALTH AND MEDICAL RESEARCH INSTITUTE
Sababu ya mlipuko wa Kaswende bado haijafahamika kikamilifu, ingawa wataalamu wanasema inaweza kwa sehemu moja na kuhama kwa watu kutoka maeneo ya jamii moja kuelekea maeneo ya jamii nyingine.
Kaswende ni nini?
- Kaswende ni ugonjwa unaoenezwa kwa maambukizi ya bakteria kwa njia ya ngono
- dalili za awali ni pamoja na kuvimba kwa sehemu za siri pamoja na mdomo, vipele mwilini, maumivu ya kichwa pamoja na viungo
- Watu wazima wanaweza kutibiwa kwa dawa za tiba ya maambukizi(antibiotics)
- Usipotibiwa yanaweza kusambaa hadi kwenye moyo, ubongon, na viungo vingine vya mwili na hata kusababisha kifo
- Wanawake wajawazito wanaweza kujifungua watoto wenye kasoro za viungo na pia mimba zinaweza kutoka
- Watoto wachanga wanaozaliwa na kaswende wanaweza kufa ama kupatwa na ulemavu wa kudumu ckama vile wa kutoona.

Chanzo cha picha, SEL
Serikali ya Australia imeelezea tatizo la maambukizi ya kaswende kama lisilokubalika , na ikakiri kwamba ilichukua muta kulitafutia ufumbuzi .
"katika siku na umri kama wetu, unaposikia hilo unafikiria: Balaa gani hili limetokea? Ni kwa vipi hali hii iliruhusiwa kutokea ?'" Ken Wyatt waziri wa afya jamii za watu asilia Australia alikiambia kituo cha habari cha Australia mapema mwezi huu.
'Aibu' ya kuomba msaada
Hatua za dharura za kukabiliana na mlipuko wa kaswende zimechukuliwa na serikalini ikiwa ni pamoja na kampeni mpya za matangazo ya biashara,zana kama za kuchukua vipimo kuwatibu wagonjwa haraka. Vifaa vya kwanza vya kuwapima wagonjwa vilisambazwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.
Hata hivyo, wahudumu wa afya wanasema mchakato wa utoaji huduma za matibabu unazuiwa mara kwa mara na hofu ya watu kujitokeza kupimwa kutokana na unyanyapaa wa jamii unaozingira ugonjwa wa kaswende.
Kuwashawishi wagonjwa kutibiwa pia ni huwa ni vigumu, anasema Marion Norrie, muhudumu wa afya wa watu wa jamii asilia kaskazini mwa Queensland.













