Unahitaji usingizi wa kiwango gani? "Usingizi mdogo unaweza pia kufupisha maisha yako"

Ni wanasiasa wangapi na wafanyabiashara utawaskia wakijigamba vile wanalala kwa muda mfupi?

Kukosa kulala usingizi wa kutosha husababisha madhara kwa ubongo wetu na miili yetu pia.

Matthew Walker ni professor ya saikolojia huko UC Berkely.

Ameandika kitabu kuhusu "Ni kwa nini Tulala" kitabu chenye uwezo wa kubadili na kurefusha maisha yako.

Anaelewa kuwa watu wana mambo mengi ya kufanya maishani lakini kutokana na ushahidi uliopo hakuna sababu yoyote kuhusu ni kwa nini hatufanyi jitihada za kuongeza muda wa kulala.

Wakati tunapigana na baolojia tunapoteza na kulingana na vile tunajua tumepoteza kwa magonjwa.

Ni kwa nini usingizi ni wa maana?

Ikiwa unataka kuishi hadi uzeeni na kuwa na afya nzuri ni lazima ulale masaa mengi iwezekanavyo, ni lazima uwekeze kwa usingizi mzuri.

Kulala ndio mfumo wa afya unaopatikana kwa njia rahisi ambao kila mtu anahitaji.

Manufaa ya kiafya yanayotokana na kulala yalichangia Prof Walker kuwashauri madaktari kuwapa ratiba ya kulala wagonjwa wao.

Lakini ni lazima uwe ni usingizi wa kawaida, kwa kuwa vidonge vya kualala vimehusishwa na saratani na hata vifo.

Kipi hutokea kwa mwili wakati hatulali?

Magonjwa ambayo huua watu kwenye nchi zinazoendelea yana uhusiano fulani na kukosa kulala yakiwemo ya moyo. uzani wa mwili kupita kiasi, kisukari, msongo wa akili na kujiua.

Kila mfumo wa mwili wa binadamu hupata kujiunda upya wakati mtu analala na mfumo huu huathirika sana wakati mtu anakosa kulala.

Ni masaa mangapi mtu anastahili kulala ili apate kuwa na afya nzuri?

Jibu fupi ni kati ya saa saba na saa tisa.

Mara unapolala chini ya saa saba, mwili wako unaanza kukumbwa na matatizo ya kiafya ikiwemo ukosefu wa kinga ya mwili.

Iwapo utashinda bila kulala kwa saa 20 mwili wako utakuwa katika hali sawa na mtu mlevi.

Moja ya tatizo la kukosa kulala ni kwamba hauwezi kugundua ni athari zipi zinazokupata.

Ni sawa na mlevi aliye kwenye baa, ambaye huchukua funguo za gari na kusema niko sawa.

Mbona tunalala muda mfupi?

1. Kukosa kujua

Licha na jamii na wanasayansi kufahamu mengi kuhusu umuhimu wa kulala, hadi sasa imeshindwa kuuhamasisha umma.

Watu wengi hawafahamu kuhusu umuhimu wa kulala kwa hivyo hawatilii maanani.

2. Hali ya maisha

Kwa jumla tunafanya kazi masaa mengi na kutumia muda mwingi kusafiri.

Tunaondoka manyumbani mapema asubuhi na kurudi jioni kabisa lakini hata hivyo hatutaki kuacha familia na maisha yetu ya kawaida

3. Imani

Ikiwa utamuambia mtu kuwa unalala masaa tisa atakutazama na kufikiria kuwa wewe ni mvivu.

Kwa hivyo suala la kulala pia huonekana kama tatizo.

Watu hutembea wakijivuna kuhusu jinsi wanalala saa chache.

4. Mazingira

Mtu uhitaji giza kuweza kutoa homoni ambazo zitasaidia katika kupata usingizi ulio mzuri.

Lakini tatizo kubwa hapa ni kwamba kila mara taa huwa zimewaka.

Mambo yanayoweza kukusaidia kupata usingizi