Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
G7 na Trump: Ni kina nani walio kwenye picha hii?
Nyakati zisizo za kawaida zilikuwa zinaratajiwa kutoka kwa mkutano wa kimataifa wa nchi tajiri zaidi duniani wa G7 na akaunti ya Istagram ya Chansela wa Ujerumani Angela Merkel imeonyesha baadhi yazo.
Hawa ni watu walio kwenye picha hizo
1. Donald Trump, Rais wa Marekani.
Trump aliwashtua washirika wa Marekani wakiwemo Muungano wa Ulaya, Mexico na Canada wakati hivi majuzi alitangaza kodi ya asilimia 25 kwa bidhaa za chuma kutoka nchi hizo. Wanatishia kulipiza kisasi na suala hilo liligubika mkutano huo na mara nyingi Trump alibaki ametengwa.
2. John Bolton, Mshauri wa usalama wa katika wa Marekani.
Imekuwa miezi mitatu tangu ateuliwe kuwa mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya usalama lakini John Bolton amekuwa mwenye ushawishi. Moja ya malalamiko ya Trump yanayohusu usalama wa kitaifa na yameungwa mkono pakubwa na Bw Bolton.
3. Kazuyuki Yamazaki, naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Japan.
Alipewa cheo hicho Julai 2017, hivi majuzi aliongoza ujumbe wa Japan nchini Pakistan na kuongeza mazungumzo kati ya Japana, China na Korea Kusini mjini Seoul kuhusu biashara.
4. Shinzo Abe, Waziri mkuu wa Japan
Amekuwa chini ya shinikizo kali kujiunga katika hatua za kulipiza kisasi kodi ya Marekani. Hii inamweka katika hali ngumu- amejaribu sana kubuni uhusiano mzuri na Donald Trump.
5. Yasutoshi Nishimura, Naibu mkuu wa baraza la mawazizi nchini Japan
Mbunge huyo kutoka chama tawala nchini Japan wakatia mmoja anifanya kazi kwenye wizara ya biashara na viwanda.
6. Angela Merkel, Chansela wa Ujerumani
Amekuwa kwenye mstari wa mbele katika kujaribu kutatua tofauti kwenye mkutano, ni bayana kwenye picha hii. Merkel alipendekeza kuwekwa mikakati yakutatua tofauti za kibiashara kati ya Marekani na washirika wake siku ya Ijumaa. Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Rais Trump Bi Merkel alisema viongozi hao hawakuwa wanakubaliana wakati wote lakini wanaweza kusameana.
7. Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa
Alijibizana vikali na Trump kwenye Tittwer kuhusu kodi saa chacahe kablaa ya mkutano na kuzua imaswa;li ikiwa uhusiano mzuri kati yao umekwisha. Licha ya hilo walionekana kuwa na uhusiano mzuri na kikosi cha rais Macron kilisema kuwa mazungumzo yake na Trump yalikuwa ya manufaa.
8. Theresa May, Waziri mkuu wa Uingereza
Wakati wa mazungumzo ya wiki iliyopita alimwambia Rais Trump kuwa kodi za Marekani zinakasirisha. Lakini alionekana kutumia lugha isiyo kali na kuwashauri viongozi kujiepusha na hatua zinazoweza kusababisha vita vya kibiashara.
9. Larry Kudlow, Mkurugenzi wa baraza la kiuchumi la Marekani
Mshauri mkuu wa masuala ya uchumi wa Trump alitetea kodi hizo mpya na kusema kuwa Trump hawezi kulaumiwa kwa msukosuko wa kibiashara. Baada ya mkutano Bw Kudlow aliiamba CNN kuwa mkutano huo ulikuwa wa nia njema