Harusi ya Kifalme 2018: Harry na Meghan watoa picha rasmi za harusi yao

Mtawala na Mke Mtawala wa Sussex, Harry na Meghan, wametoa picha rasmi za harusi yao ambayo ilifanyika Jumamosi.

Picha hizo ambazo zilipigwa na Alexi Lubomirski zinajumuisha picha moja ya pamoja inayowashirikisha watoto waliosimamia harusi hiyo pamoja na jamaa za karibu, wakiwemo wazazi na Malkia.

Wawili hao wangependa kushukuru kila mmoja aliyehudhuria sherehe yao Jumamosi, Kasri la Kensington imesema.

"Wamefurahishwa sana na picha hizi rasmi," taarifa hiyo imeongeza.

Bw Lubomirski, aliyepiga picha rasmi za kuchumbiana kwa wawili hao alisema imekuwa heshima kubwa kwake kupiga picha na kunakili "safari yao ya mapenzi".

"Hii imekuwa sura ya kupendeza sana katika maisha yangu kikazi na kimaisha, ambayo sitaisahau kamwe," amesema.

.