Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ugaidi wahusishwa na ghasia za Israel
Jeshi nchini Israel limerusha video fupi inayomuonesha mwanachama mwandamizi wa Hamas akionekana kusema kuwa Wapalestina hamsini waliouawa na Israeli katika ukanda wa Gaza mwanzoni mwa wiki hii walikuwa wanamgambo wa dola ya Kiislam.
Msemaji wa Waziri Mkuu wa Israel anasema ni ushahidi kwamba hayakuwa maandamano ya amani bali harakati za kundi la Hamas.
Ofir Gendelman anasema kwamba Israeli itawasilisha mara moja video hiyo kama ushahidi kwa jumuiya ya kimataifa kuwa maandamano yalikuwa ni mwavuli uliogubika ugaidi.
Israeli imekabiliwa na upinzani mkubwa wa kimataifa juu ya mwenendo wa askari wake mwanzoni mwa juma hili, huku nchi kadhaa ulimwenguni zikitaka uchunguzi huru na wa haki tena wa kujitegemea dhidi ya tukio hilo.