Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wajawazito Ghana watumia vidonge vya kuwachubua ngozi watoto tumboni
Wanawake nchini Ghana wameonywa kutotumia dawa za kujichubua ilikubadilisha ngozi ya watoto kuwa nyeupe wakati bado wako tumboni.
Wataalam wa afya wanasema dawa hizo haramu zinapelekea madhara ya uzazi ikiwemo viungo vya ndani vya mtoto kuharibika.
Mamlaka ya Vyakula na Dawa Ghana (FDA) imesema utumiaji ya vidonge vya Glutathione ni hatari ikiongezea kuwa inataka " umma ifahamu kuwa hamna dawa zilizoruhusiwa na FDA aina ya vidonge vya kuchubua ngozi ya mtoto aliye tumboni"
Vitendo vinashamiri nchini Ghana, kwa mujibu wa FDA, mara nyingi vidonge vinaingizwa kinyemela ndani ya mizigo kwa viwango vikubwa kupitia viwanja vya ndege.
Polisi na vikosi vya usalama wanafanya kazi pamoja kuwashika na kuwashtaki makampuni na watu binfsi watakaokuwa na vidonge visivyoruhusiwa.