Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
ANC chaadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela
Chama tawala cha Africa Kusini ANC kimeanza maadhimisho ya kumbukumbu za miaka mia moja tangu kuzaliwa kwa Raisi wa kwanza mweusi nchini humo shujaa Nelson mandela.
Kiongozi wa sasa wa ANC ,Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutoa hotuba huko medani mwa Freedom square mjini Cape Town, ambako marehemu Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza alipoachilia huru kutoka gerezani miaka ishirini na nane iliyopita.
Rais Jacob Zuma ambae anakabiliwa na madai chungu nzima ya rushwa amegoma kubanduka huku shinikizo za kumtaka ajiuzulu zikizidi kumzonga .
ANC imetangaza mkutano maalum wa kamati yake kuu ya kitaifa utafanyika Jumatatu kujadili swala hilo.