Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri afya
Ripoti mpya ya mabadiliko ya hali ya hewa imeonyesha kuwa kuongezeka kwa joto kunaathiri afya ya binaadam kwa kiasi kikubwa.
Ripoti hizo kutoka kundi la vyuo mbalimbali na mashirika tofauti ya umoja wa mataifa zinasema watu wengi wanaathirika na joto pamoja na mlo hafifu sambamba na kusambaa kwa magonjwa.
Katika toleo la Lancet wamesema njaa kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na ongezeko la joto linalopelekea mimea kukauka.
Wameonyesha pia uwezekano wa kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa malaria kutokana na mazingira kutokuwa safi.