Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri afya

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa
Maelezo ya picha, Athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Ripoti mpya ya mabadiliko ya hali ya hewa imeonyesha kuwa kuongezeka kwa joto kunaathiri afya ya binaadam kwa kiasi kikubwa.

Ripoti hizo kutoka kundi la vyuo mbalimbali na mashirika tofauti ya umoja wa mataifa zinasema watu wengi wanaathirika na joto pamoja na mlo hafifu sambamba na kusambaa kwa magonjwa.

Viwanda vinatajwa kwa kiwango kikubwa kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa
Maelezo ya picha, Viwanda vinatajwa kwa kiwango kikubwa kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa

Katika toleo la Lancet wamesema njaa kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na ongezeko la joto linalopelekea mimea kukauka.

Wameonyesha pia uwezekano wa kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa malaria kutokana na mazingira kutokuwa safi.