Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ulinzi waimarishwa Cameroon
Polisi na wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mitaani katika mikoa ya Cameroon inayozungumza lugha ya Kiingereza, baada ya kutokea ghasia zilizosababisha vifo siku ya Jumapili.
Vurugu hizo zilitokea kati ya vyombo vya usalama na watu wanaodai uhuru.
Kiongozi wa upinzani nchini humo, John Fru Ndi ameiamba BBC kwamba watu 30 wameuawa katika mapigano yaliyosababishwa na vurugu hizo, ingawa vyanzo vingine vya habari vinasema ni watu saba tu waliothibitishwa kufariki dunia.
Katika mji wa Bamenda, Kaskazini Magharibi mapambano yanaripotiwa kuendelea kati ya vijana na polisi wa kuzuia ghasia ambao walikuwa wakipiga mabomu ya kutoa machozi.
Jamii ya wa Cameroon wanaozungumza lugha ya Kiingereza ambao ni wachache wamekuwa wakiandamana karibu mwaka mzima kupinga kile wanachosema kubaguliwa katika elimu na mfumo wa sheria.