Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Korea Kaskazini yaongezwa kwenye zuio la kuingia Marekani
Marekani imepitisha vikwazo vipya vya zuio la kuingia nchini humo,ikiiongeza nchi ya Korea kaskazini raia wake kutoingia katika taifa hilo ambapo mengine yaliyoingizwa katika vikwazo hivyo ni Venezuela na Chad .
Sababu zilizopelekea Marekani kuweka vikwazo kwa raia wa nchi hizo kuingia nchini humo ni pamoja na usalama wa nchi zao kuwa duni na ukosefu wa ushirikiano.
Hatua hiyo ya Marekani imetoa masharti tofauti kati ya nchi na nchi ambapo Venezuela,wale waliozuiwa ni wafanyakazi wa serikali na familia zao.
Sudan nayo imeondolewa katika nchi sita za kiisamu ambazo Rais Trump alikuwa ameziwekea vikwazo.
Nchi ambazo bado ziko kwenye marufuku ya Rais Trump ni pamoja na Iran,Libya,Somalia na Yemen.