Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Utafiti: Kilimo cha kupindukia chanzo cha majangwa
Utafiti wa umoja wa mataifa umebaini kuwa thuluthi moja ya ardhi kote duniani imeharibiwa na shughuli nyingi za kilimo kupindukia
Utafiti huo unaonyesha kwamba udongo usiokuwa na rutuba unatishia kuzua baa la njaa kwa mamilioni ya watu pamoja na kuleta umaskini na mizozo.
Umoja wa mataifa unasema tani bilioni ishirini na tano za udongo wenye rutuba na miti bilioni kumi na tano hupotea kila mwaka.
Umesema kuwa sera za kitaifa za kuzuia ardhi kubadilika na kuwa jangwa ni muhimu katika kuzuia kile inachodai huenda kikawa chanzo cha migogoro lakini ukaongezea kuwa uhifadhi wa chakula pia unaweza kusaidia.
Utafit huo umebaini kwamba ukulima unaofanywa na viwanda ambapo mashine kubwa hutumiwa kulima na kuvuna hupunguza rutuba ya udongo kwa kiwango kikubwa.