Mwanafunzi anayeshukiwa kuanzisha moto shuleni Nairobi afikishwa mahakamani

Msichana mmoja wa shule amefikishwa mahakamni katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kwa kushukiwa kuanzisha moto uliotokea kwenye shule moja mwishoni mwa wiki iliyipita ambapo wanafunzi 9 walifariki.

Msichana huyo amefikiswa katika mahakama inayohudumia kesi za watoto kwa sababu bado hajahitimu umri wa maika 18 ya kushtakiwa katika mahakama ya kawaida.

Jaji ameamua kuwa msichana huyo atazuiliwa korokoroni kwa muda wa siku 7 wakati uchunguzi ukiendelea kufanywa

Siku ya Jumatatu waziri wa elimu Fred Matiangi alisema kwa kisa hicho cha shule ya wasichana ya Moi hakikuwa ajali bali kilisabishwa makusudi.

"Kumekuwa na misururu ya visa kama hivyo vya moto shuleni sehemu kadhaa za kenya,

"Uchunguzi zaidi umefanyika na ninaweza kuwambia baada ya kushauriwa na polisi kuwa ile haikuwa ajali," Matiang'i aliuambia mkutano wa waandishi wa habari