Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Zaidi ya wanuame 40 waliopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja kufikishwa mahakamani Nigeria
Polisi katika mji wa Lagos nchini Nigeria wanatarajiwa kuwafikisha mahakamani zaidi ya wanaume 40 hii leo baada ya wanaume hao kukamatwa kwa vitendo vinavyodaiwa kuwa vya mapenzi ya jinsia moja mwishoni mwa wiki.
Wanaume hao walikamatwa katika hoteli moja iliyo mtaa wa Owode Onirin mjini Lagos kulingana na vile magazeti kadhaa yalivvyomnukuu msemaji wa polisi.
Olarinde Famous-Cole aliongeza kuwa hoteli hiyo imefungwa huku uchanguzi ukiendelea