Mtu tajiri zaidi barani Asia Jack Ma ziarani Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtu tajiri zaidi barani Asian Jack Ma, yuko nchini Kenya wakati anapoanza ziara yake katika nchi za Afrika Mashariki.
Bwana Ma ambaye anamiliki kampuni ya Alibaba ambayo inaripotiwa kumiliki asilimia 11 ya biashara ya mtandao nchini China, atawahutubia vijana mjini Nairobi kabla ya kuelekea nchini Rwanda kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Anaoandamana nao katika ziara hiyo ni kundi la wafanyabiashara matajiri wa kichina ambao wanatafuta fursa za uwekezaji.

Chanzo cha picha, Getty Images








