Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Madonna azuia mnada wa barua ya uhusiano wake na Tupac Shakur
Jaji mmoja nchini Marekani amesitisha mnada wa vitu binafsi vya mwanamuziki Madonna baada ya kusema kuwa haki yake ya faragha ilikiukwa.
Jaji wa mji wa New York Gerlad Lebovits aliamuru kesi hiyo kusikizwa kikamilifu mnamo mwezi Septemba tarehe 6, akilizuia jumba litakalofanya mnada huo la Gotta have Rock kuendelea na biashara hiyo.
Chupi ya Madonna, kitabu cha hundi , kichana , picha na barua ya uhusiano kati ya msanii huyo na aliyekuwa mwanamuziki Tupac Shakur ni miongoni mwa vitu vilivyosimamishwa kupigwa mnada.
Madonna anasema kuwa vitu hivyo viliibwa na rafikiye wa zamani.
Barua hiyo ya Tupac ambapo Tupac anasema kuwa uhusiano wake na Madonna ulivunjika kutokana na ubaguzi wa rangi ilitarajiwa kuuzwa kwa dola 400,000.
Barua hiyo ni ya tarehe 15 mwezi Januari 1995 na iliandikwa na Tupac Shakur wakati alipokuwa akihudumia kifungo cha miezi 18 kabla ya kupigwa risasi na kuuawa.
Wasanii wote wawili walikuwa maarufu sana wakati huo.