Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kenya yaagiza mahindi kutoka Ethiopia
Kenya imeanza kuagiza mahindi kutoka taifa jirani la Ethiopia kutokana na uhaba mkubwa wa nafaka hiyo.
Malori ambayo yamebeba zaidi ya tani 260 za mahindi yaliwasili katika mji wa mpakani wa Moyale leo.
Malori mengine yanatarajiwa kuwasili baadaye wiki hii.
Mahindi hayo yamenunuliwa na Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Kenya.
Ethiopia inadaiwa kupata $21.3m kutokana na uuzaji wa mahindi hayo.
Gazeti la kibinafsi la Addis Fortune hata hivyo limeshangaa ni kwa nini Ethiopia inauza mahindi nje ilhali kuna maeneo mengine yanayokabiliwa na baa la njaa.