Picha za aliyefanya shambulizi Manchester zatolewa

Picha za Salman Abedi

Chanzo cha picha, Greater Manchester Police

Maelezo ya picha, Picha za Salman Abedi

Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.

Maeneo 14 yanasakwa na wanaume 11 wamekamtwa kwa kushukiwa kuhusika katika ugaidi.

Abedi alitambuliwa saa mbili baada ya shambulizi la siku ya Jumatatu.

Waziri mkiu Theresa May anasema kuwa kiwango cha tisho lililopo kimepunguzwa na wanajehsi waliotumwa kuwasaidia polisi wataondolewa kuanzia siku ya Jumatatu

Police

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ulinzi mkali uliwekwa Wembley

Mamia ya polisi waliojihami wanaendelea kulinda mamia ya tamasha kote nchini Uingereza.

Mamia ya polisi walitumwa wakati mashabiki 50,000 walihudhuriw tamasha la Courteeners kwenye uwanja wa kriketi wa Old Trafford, ambalo ni tamasha kubwa kufanyika mjini humo tangu shambulizi kutokea.

Ulinzi zaidi umewekwa leo wakati wa mbio za Great Manchester Run ambapo maelfu ya wanariadha wanatarajiwa kushirikia

Police put up a corden as they attend the scene of a raid in the Moss Side area of Manchester

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku ya Jumamosi polisi walivamia eneo la Moss Side huko Manchester