Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bomba la kupitisha pombe kujengwa Ujerumani
Waandalizi wa Tamasha maarufu la muziki wa rock nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja zaidi ya elfu 75 kwamba, katu! hawatokumbwa na kiu ya pombe.
Wanajenga bomba kubwa la kusafirisha pombe katika eneo la tamasha hilo.
Waandalizi wa tamsha hilo maarufu kwa jina, Wacken Open Air festival, wanasema bomba hilo litakuwa na uwezo wa kufikisha glasi sita za pombe kwa kila sekunde.
Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na upana wa inchi 14.
Watu elfu 75 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwaka, na inakadiriwa kwamba kila mmoja huwa anabugia lita tano za pombe katika kipindi cha siku tatu.