Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Muungano wa wafanyikazi wampiga marufuku rais Zuma
Baraza la Muungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu ambalo ni mshirika mkuu wa chama tawala cha ANC limempiga marufuku rais Jacob Zuma kuhutubia katika mikutano yake.
Akisoma taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne baada ya mkutano mkuu wa baraza hilo, katibu mkuu wa Cosatu Bheki Ntshalintshali alisema: Rafiki Jacob Zuma hataruhusiwa tena kuhutubia katika Cosatu.
Bwana Zuma alizomwa katika mkutano wa wafanyikazi wa mwezi Mei ulioandaliwa na Cosatu mapema mwezi huu.
Chama cha ANC kimegawanyika kabla ya kufanyika kwa mkutano wake wa kila mwaka ambapo rais Zuma anatarajiwa kujiuzulu kama kiongozi wa chama.
Muungano huo ambao ni mkubwa umesisitiza wito wake kwamba haumuungi mkono tena rais Zuma.