Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Yahya Jammeh aliiba dola milioni 50 kutoka kwa serikali
Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh aliiba takriban dola milioni 50 kutoka kwa taifa kabla ya kuondoka nchini humo mwezi Januari, kwa mujibu wa waziri wa sheria.
Jammeh analaumiwa kwa kuiba pesa hizo kupitia kwa kampuni ya mawasiliano ya serikali.
Kwa sasa mahakama imeagiza kutwaliwa kwa mali yake yote yaliyosalia nchini Gambia.
Jammeh alikimbia kuenda nchini Equitorial Guinea baada ya miaka 22 uongozini.
Alishindwa kwenye uchaguzi mwezi Disemba na baadaye kukubali kuondoka madarakani baada ya vikosi vya eneo ilo kutishia kumuondoa madarakani.
Magari ya kifahari na bidhaa zingine ziliripotiwa kuingiza kwenye ndege ya mizgo ya Chad wakati Jammeh alikuwa akiondoka nchini humo.
Pesa hizo zilitajwa kuwa dola milioni 11 na waziri wa masuala ya ndani Mai Ahmad Fatty, ambaye wakati huo alikuwa msaidizi wa rais Adama Barrow.
Lakini siku ya Jumatatu waziri wa sheria Abubacarr Tambadou, alisema kuwa bwana Jammeh aliiba dola milioni 50 kati ya mwaka 2006 na 2016.